Pata taarifa kuu

Coronavirus DRC: Wafanyakazi wa afya katika mkoa wa Kivu Kusini wahofia maisha yao

Madaktari na wauguzi katika Jimbo la Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanasema wanahatarisha maisha yao katika vita dhidi ya virusi vya Corona, kutokana na ukosefu wa  vifaa vya kujikinga na mazingira magumu ya kufanya kazi.

Hôpital Général de référence de Bukavu, moja ya hospitali kuu zinazopatikana mjini Bukavu.
Hôpital Général de référence de Bukavu, moja ya hospitali kuu zinazopatikana mjini Bukavu. RFI/Assétou Samaké
Matangazo ya kibiashara

Kinacho wapa hofu ni hasa ongezeko la haraka la visa vya ugonjwa wa Corona katika Mkoa wa kKvu Kusini ambao kwa sasa umethibitisha idadi ya wagonjwa 193.

Kiongozi wa chama cha madaktari katika Mkoa wa Kivu Kusini, Fabrice Cikomola, akiongea kwa niaba ya wote wanaohusika kutoa matibabu, amesema kwamba madaktari, wafamasia na wauguzi wanalalamika juu ya ukosefu wa kinga dhidi ya maambukizi ya Corona.

“18% ya wagonjwa wa Covid-19 ni waganga. Ilikuwa 43% wiki mbili zilizopita. Yaani ikiwa kuna wagonjwa 2, mmoja ni mfanyakazi wa afya. Haiwezekane! Madaktari 5 walifariki hapa kumepita wiki mbili, amesema Fabrice Cikomola

Daktari Cikomola anafafanua kwamba wahudumu wa afya wanahitaji vitu 3 mhimu:

"Kwanza ni mafunzo, pili ni vifaa muhimu na tatu tunaomba kuwe posho kidogo, " ameongeza

Mkuu wa kitengo cha afya katika mkoa wa kivu kusini, Daktari Gaston Lubambo, anawataka wale wotewanaohudumu katika sekta ya afya katika vita dhidi ya Corona wawe na subira, huku akibaini kwamba watambua changamoto zinazowakabili na kuongeza kuwa suluhisho litapatikana.

“Ni 13% ya wafanyakazi wa afya walioambukizwa. Tunaimarisha uwezo wa wauguzi na madaktari na kuwapa vifaa. Tulipata ahadi kutoka kwa serikali ya mkoa na serikali kuu itasaidia kutafutia suluhu madai ya wafanyakazi. "

Wafanyakazi wa katika sekta ya afya wanapanga kukabidhi baruwa inayoeleza wazi madai yao kwa gavana wa Mkoa wa Kivu Kusini Jumanne wiki hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.