Pata taarifa kuu
CHINA-AFRIKA-UCHUMI

China kufuta baadhi ya mikopo kwa mataifa ya Afrika

China imesema itafuta mikopo isiyokuwa na faida iliyokuwa kama mzigo kwa mataifa mbalimbali ya Afrika wakati huu bara hilo linalopoendelea kukabiliana na janga la Corona.

Uhuru Kenyatta (safu ya pili kushoto) na marais wenzake wa Kiafrika na rais wa China Xi Jinping kwenye mkutano wa kilele kati ya China na Afrika Septemba 3, 2018.
Uhuru Kenyatta (safu ya pili kushoto) na marais wenzake wa Kiafrika na rais wa China Xi Jinping kwenye mkutano wa kilele kati ya China na Afrika Septemba 3, 2018. HOW HWEE YOUNG / POOL / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais Xi Jinping ametoa tangazo hilo na kuongeza kuwa mataifa yaliyoatiriwa zaidi na virusi hivyo vitapewa muda wa kulipa madeni wanayodaiwa.

Akizungumza na viongozi wa nchi hizo kupitia mfumo wa Video, rais Jinping pia amezitaka taasisi za fedha za China kuwa na mazungumzo ya kirafiki na nchi za Afrika kuona namna watakavyolipa madeni yao.

Aidha, katika hatua nyingine, amesema nchi yake itasimama na bara la Afrika katika vita dhidi ya Corona na kufadhili ujenzi wa makao makuu ya kudhibiti magonjwa barani Afrika jijini Addis Ababa.

Bara la Afrika kwa sasa lina maambukizi zaidi ya Laki Mbili na vifo zaidi ya Elfu saba kutokana na janga la Corona.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.