Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-MAJANGA YA ASILI

Mji wa kiuchumi wa Côte d’Ivoire wakumbwa na mafuriko mabaya

Mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni katika mji mkuu wa kiuchumi wa Côte d’Ivoire, Abidjan, imesababisha mafuriko katika maeneo mengi ya mji huo na kusababisha watu wengi kuyahama makazi yao.

Katika miaka ya hivi karibuni, mafuriko yamekuwa yameendelea katika baadhi ya maeneo ya mji wa Abidjan, kama eneo hili hapa ilikuwa mwaka 2018. (picha ya kumbukumbu)
Katika miaka ya hivi karibuni, mafuriko yamekuwa yameendelea katika baadhi ya maeneo ya mji wa Abidjan, kama eneo hili hapa ilikuwa mwaka 2018. (picha ya kumbukumbu) Sia KAMBOU / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mvua hiyo imesababisha mtu mmoja kupoteza maisha, msichana wa miaka 6, na kuwajeruhi watu wengine wengi, huku nyumba na maduka kuharibika vibaya. Wilaya za André Château d'Eau, Abobo-Belleville na Riviera Palmeraie zimeathirika zaidi kutoka na mvua hiyo.

Kila mwaka, wakati wa msimu wa mvua, eneo la Riviera Palmeraie huathirika zaidi kutokana na kuongezeka kwa viwango vya maji. Baadhi ya maeneo yalikumbwa na mafuriko mara tano katika miaka ya hivi karibuni.

Kwa sasa serikali imeweka nambari kadhaa za dharura ambazo watu wametakiwa kupiga ikiwa kutatokea mtukio mbalimbali yanayohusiana na mafuriko.

Mvua inatarajiwa kuendelea kunyesha wiki hii yote, mamlaka ya hali ya hewa Sodexam, imeonya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.