Pata taarifa kuu
DRC-EBOLA-AFYA

DRC yaendelea na zoezi la kutoa chanjo kwa raia wake dhidi ya Ebola

Wizara ya afya nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imesema imeanza kutoa Chanjo ya kuzuia kuenea kwa virusi vya Ebola katika eneo la Kaskazini Magharibi mwa taifa hilo.

Mwanamke huyu na mtoto wake wakisubiri kupewa chanjo dhidi ya Ebola. Goma, DRC, Agosti 5, 2019.
Mwanamke huyu na mtoto wake wakisubiri kupewa chanjo dhidi ya Ebola. Goma, DRC, Agosti 5, 2019. REUTERS/Baz Ratner/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Akiwa ziarani katika mji mkuu wa Mbandaka kwenye Jimbo la Equateur waziri wa Afya, Dk Eteni Longondo, ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kuwa wahudumu wa afya, wameanza kutoa chanjo hiyo tangu siku ya ijumaa wiki iliyopita wakipata msaada mkubwa kutoka kwa washirika wa karibu wa kimataifa kuhusu masuala ya afya.

Dokta Longondo amesema madaktari pamoja na wahudumu wengine wa afya ndio ambao walikuwa mstari wa mbele kupewa chanjo hiyo kabla ya kuwaendea wakaazi wa eneo hilo.

Kipimo cha mwanzo kilichokuwa kimepelekwa huko Mbandaka kilikadiriwa kuwa dozi elfu moja na mia tano ambapo walihitaji dozi zaidi ya elfu nane, alisema waziri Longondo.

Mji wa Mbandaka ni mji Mkuu wa Mkowa wa Equateur nao umeshuhudia visa vipya 12 vya maambukizi ya ugonjwa hatari wa Ebola, ambapo Mlipuko wa kumi na moja wa Ebola ulitangazwa Juni 1, na tangu kuripotiwa kwa ebola huko Equateur kati ya mwezi Mei na Julai 2018 ni wagonjwa 33 ndio wamefariki dunia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.