Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-HAKI

Waziri wa zamani wa Ulinzi wa Burkina Faso Jean-Claude Bouda azuiliwa jela

Waziri wa zamani wa Ulinzi wa Burkina Faso Jean-Claude Bouda yuko mikononi mwa vyombo vya dola tangu Jumanne Mei 26 katika mji mkuu wa nchi hiyo, Ouagadougou.

Waziri wa zamani wa Ulinzi wa Burkina Faso Jean-Claude Bouda alipelekwa moja kwa moja kizuizini jijini Ouagadougou baada ya kupatikana na hatia ya utakatishaji wa fesha na makosa mengine.
Waziri wa zamani wa Ulinzi wa Burkina Faso Jean-Claude Bouda alipelekwa moja kwa moja kizuizini jijini Ouagadougou baada ya kupatikana na hatia ya utakatishaji wa fesha na makosa mengine. © Doug Berry/Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kusikilizwa kufuatia malalamiko kutoka kwa shirika linalopambana dhidi ya ufisadi kuhusu makosa ya utakatishaji wafedha na kujitajirisha kinyume cha sheria, waziri huyo wa zamani alipelekwa moja kwa moja kizuizini jijini Ouagadougou.

Kwa mujibu wa mwanshi wetu huko Ouagadougou Yaya Boudani, kesi hiyo ilianza mwezi Desemba 2018. Picha za nyumbaya kifahari ya waziri wa zamani wa ulinzi zimeibua maswali mengi nchini Burkina Faso. Miezi michache baadaye, shirika linalopambana dhidi ya ufisadi liliwasilisha mahakamani malalamiko kuhusu vitendo vya uhalifu wa utakatishaji wa fedha na kujitajirisha kinyume cha sheria, ambavyo ni miongoni mwa mashitaka yanayomkabili.

Shirika la REN-LAC limeeleza kuwa kupatikana kwa mali hii isiyohamishika, ambayo thamani yake inakadiriwa karibu pesa za CFA nusu bilioni, haikuonekana popote pale kwenye taarifa ya waziri huyo wa zamani alipotangaza mali yake wakati alipoteuliwa kushikilia wadhifa huo serikalini. "Na rasilimali ambazo alitangaza hazingemuwezesha kupata nyumba hiyo ya kifahari," shirika la REN-LAC limebaini.

Baada ya kusikilizwa na mahakama, Waziri wa zamani wa ulinzi wa Burkina Faso Jean-Claude Bouda alipelekwa kizuizini huko Ouagadougou. Kulingana na chanzo cha mahakama, anashitakiwa makosa ya "kughushi , utakatishaji wa fedha, na kosa la la kudanganya". Jina lake pia limetajwa katika kesi zingine ambazo malalamiko hayajawasilishwa mpaka sasa mahakamani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.