Pata taarifa kuu
DRCKABUND-HAKI-SIASA

DRC: Jean-Marc Kabund atimuliwa kwenye wadhifa wake bungeni

Kaimu kiongozi wa chama cha rais cha UDPS, Jean-Marc Kabund, ametimuliwa kwenye wadhifa wake kama naibu wa kwanza wa spika wa Bunge la taifa. Uamuzi ambao ulichukuliwa Jumatatu jioni wiki hii.

(Picha ya kumbukumbu) Jean-Marc Kabund (kulia), Januari 2019.
(Picha ya kumbukumbu) Jean-Marc Kabund (kulia), Januari 2019. AFP PHOTO/ Caroline Thirion
Matangazo ya kibiashara

Bw. Kabund alitimuliwa kwenye wadhifa wake baada ya hoja iliyoletwa bungeni na Jean-Jacques Mamba, mbunge wa chama cha MLC kupigiwa kura.

Chanzo cha kesi hiyo ni pendekezo la rais wa Bunge la Seneti na spika wa Baraza la Wawakilishi la kuitisha kikao ili kurasimisha hali ya dharura ya afya iliyotangazwa na rais Félix-Antoine Tshisekedi mwezi Machi.

Kwa mujibu wa mwandishi wetu DRC Kamanda wa Kamanda Muzembe Jean-Marc Kabund aliondolewa kwenye wadhifa wake baada ya hoja ya Jean-Jacques Mamba kupigiwa kura nying sawa na kura 289 kwa jumla ya kura 315.

Jean-Jacques Mamba alimshtumu Jean-Marc Kabund, kaimu kiongozi wa chama cha rais cha UDPS, kwamba alichafua taswira ya Bunge la Kitaifa kwa madai kwamba Jean-Jacques Mamba alikuwa alisema "uwongo".

Muda mfupi baada ya kuomba kufukuzwa kwa Jean-Marc Kabund, Jean-Jacques Mamba alikamatwa mwishoni mwa wiki iliyopita ... Vyombo vya sheria vilimfungulia mashitaka na kumuweka chini ya kifungo cha nyumbani, vikimtuhumu kosa la kughushi saini kuhusu ombi lake ambalo lilikuwa limepitwa na wakati.

Uingiliaji huu wa vyombo vya sheria katika mambo ya bunge haukuthaminiwa katika Bunge la kitaifa. Spika wa Baraza la Wawakilishi, Jannine Mabunda, na wabunge wengine kadhaa, muungano wa vyama vinavyoshiriki serikalini na upinzani kwa pamoja walitaka kuachiliwa huru kwa Jean-Jacques Mamba.

Tume iliyoundwa kwa sababu hii ilihitimisha kuwa saini iliyotiliwa kwenye waraka ilikuwa halali. Na mvutano kati ya wabunge kadhaa katika kikao hicho cha bunge haukuzuia kura kupigwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.