Pata taarifa kuu
TUNISIA-CORONA-AFYA-UCHUMI

Coronavirus: Tunisia kuanza kulegeza masharti ya watu kutotembea

Waziri wa afya nchini Tunisia, Abdelatif El-Makki, amesema taifa hilo limefanikiwa kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona, na serikali inapanga kuondoa baadhi ya marufuku ya watu kutotembea.

Pwani tupu huko Hammamet, baada ya serikali ya Tunisia kuweka marufku ya kutotembea katika kudhibiti ugonjwa wa Covid-19, mnamo Machi 2020.
Pwani tupu huko Hammamet, baada ya serikali ya Tunisia kuweka marufku ya kutotembea katika kudhibiti ugonjwa wa Covid-19, mnamo Machi 2020. REUTERS/Zoubeir Souissi
Matangazo ya kibiashara

Abdelatif El-Makki pia amesema baadhi ya kampuni na migahawa zitaruhusiwa kufanya kazi kuanzia wiki ijayo. Tunisia imethibitisha visa 1000 vya maambukizi pamoja na 40 kutokana na Corona.

Maambukizi ya virusi hivi barani Afrika yamefikia zaidi ya Elfu 35 na vifo zaidi ya Elfu moja na 500.

Mapema Mwezi wa Aprili mwaka huu, rais wa Tunisia Kaïs Saïed aliagiza kuachiwa huru wafungwa 1,420 kufuatia maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo.

Machi 20 rais wa Tunisia alitangaza karantini nchini humo ikiwa ni katika jitihada za kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona na kuwataka wananchi wasalie majumbani kwao isipokuwa katika masuala ya dharura.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.