Pata taarifa kuu
ECOWAS-CORONA-AFYA

Coronavirus: Viongozi wa ECOWAS wakutana kuzungumzia hali halisi

Viongozi wa nchi na serikali wanatarajia kukutana kupitia video ili kujadili hali halisi kuhusu janga la kimataifa la Covid-19.

Marais na wakuu wa serikali za nchi za Jumuiya ya Kiuchumi Afrika Magharibi wanakutana huko Abuja, Desemba 16, 2015. (Picha kumbukumbu)
Marais na wakuu wa serikali za nchi za Jumuiya ya Kiuchumi Afrika Magharibi wanakutana huko Abuja, Desemba 16, 2015. (Picha kumbukumbu) REUTERS/Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Huu ni mkutano wa kwanza tangu kuzuka kwa janga hili katika ukanda huo.

Rais wa Niger, Mahamadou Issoufou, ndiye atafungua mkutano huo, ambao viongozi wa nchi na serikali za jumuiya hiyo ya kiuchumi ya Afrika Magharibi, wamesema watashiriki.

Hivi karibuni kiongozi mkuu wa Afrika katika Shirika la Afya Duniani, Matshido Moeti alisema virusi vya corona "havitasababisha maelfu ya vifo pekee" barani Afrika, bali pia huenda vikaathiri pakubwa "uchumi na ustawi wa kijamii".

Benki ya dunia inasema athari zinazotokana na ugonjwa wa Covid-19 katika bara hilo zimegawanyika katika sehemu tatu:

  • Biashara zimeathirika na kushindwa kusafirishwa kwa bidhaa
  • Fedha za ufadhili kupungua na hata fedha kutoka nchi za kigeni kupungua
  • Matatizo ya kila siku katika uchumi yanayosababishwa na makatazo mbalimbali na watu kufungiwa

Afrika imethibititsha visa zaidi ya 10,000 vya virusi vya corona pamoja na vifo zaidi ya 500 kulingana na Kituo cha Udhibiti na Uzuiaji wa Magonjwa (ACDC).

Huku idadi ya wanaoambukizwa ikiongezeka kila siku, baadhi wanahofia kwamba kitovu cha virusi hivyo huenda kukahamia barani Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.