Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-USALAMA

DRC: Mvutano mpya waibuka kati ya Bunge na Rais Tshisekedi

Rais wa DRC Félix Tshisekedi ameandikia rasmi Bunge na Baraza la Seneti vya nchi hiyo akiomba kuongezwa muda wa hdarura ya kiafya ambao unamalizika Aprili 24 mwaka huu.

Raisa wa DRC Félix Tshisekedi.
Raisa wa DRC Félix Tshisekedi. Sumy Sadurni / AFP
Matangazo ya kibiashara

Bunge la Kitaifa na Baraza la Seneti hatimaye wakubali kanuni ya kukutana kwa kutokaribiana na sio kwa mkutano kama walivyotaka. Lakini, mijadala hii inafanyika katika mazingira tete.

Katika agizo la Aprili 19, lililosainiwa na rais Félix Tshisekedi, inatajwa kwamba Bunge na Baraza la Seneti vinaweza tu kukutana ili kuamua "kwa ombi la idhini ya kuongezwa muda wa dharura ya kiafya iliyotangazwa Machi 24" . Maneno hayo yanaziweka tumbo joto taasisi hizo mbili zinazowakilisha raia.

Wawakilishi hao wa raia wamebaini kwamba Félix Tshisekedi hana haki ya kurekebisha ajenda ya Bunge au kuweka kikomo uhuru wa maseneta na wabunge kukutana hata wakati wa hali ya dharura.

Baadhi ya wabunge, wengi wao kutoka muungano wa vyama ninavyomuunga mkono rais wa zamani Joseph Kabila, FCC, wameomba taasisi zote mbili (Bunge la Baraza la Seneti) kutoa kuonyesha wazi msimamo wao wa kutounga mkono maneneno hayo.

Hali hii inakuja wakati ambapo pia kunaripotiwa hali ya kutoaminiana kati ya muungano wa FCC na Muungano wa CACH) wa Félix Tshisekedi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.