Pata taarifa kuu
DRC-CORONA-AFYA

DRC: Marufuku ya kutoka nje kuanza kutekelezwa katika Wilaya ya Gombe Aprili 6 hadi 20

Serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza kwamba hakutakuwa na marufuku ya kutoka nje katika mji mkuu Kinshasa ispokuwa katika wilaya ya Gombe, moja ya wilaya zinaounda mji huo; Tangazo hilo limetolewa baada ya viongozi wote kukubaliana hoja hiyo.

Moja ya maeneo ya Wilaya ya Gombe, Kinshasa, DRC.
Moja ya maeneo ya Wilaya ya Gombe, Kinshasa, DRC. Vberger/CC/Wikimedia Commons
Matangazo ya kibiashara

Mamlaka nchini DRC wanachukulia wilaya ya Gombe kama kitovu cha janga hilo ambalo tayari limeua watu 13 kati ya 134 waliotbitishwa kuambukizwa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19 kutoka mikoa mitatu ikiwa ni pamoja na mji mkuu Kinshasa, kulingana na takwimu rasmi za hivi karibuni.

Wiki iliyopita Gavana wa Mkoa wa Kinshasa alitangaza marufuku ya kutoka nje kwa jumla ya wakazi wa mkoa huo kabla ya kurejelea uamuzi wake, hali ambayo ilizua sintofahamu.

Gavana wa Mkoa wa Kinsaha, Gentiny Ngobila, amehakikisha kwamba hatua hiyo imechukuliwa baada ya mamalaka zote nchini humo kufikia makubaliano.

Kwa muda wa wiki mbili hakuna mtu atakaye ruhusiwa kuingia au kutoka katika Wilaya ya Gombe ispokuwa tu wafanyakazi wa afya na waandishi wa habari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.