Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-OUATTARA-SIASA-USALAMA

Cote d'Ivoire: Amadou Gon Coulibaly kuwania katika uchaguzi wa urais kwa tiketi ya chama cha RHDP

Rais wa Cote d'Ivoire Alassane Ouattara ametangaza kwamba anamuunga mkono Waziri wake Mkuu Amadou Gon Coulibaly kwa kuwania katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Amadou Gon Coulibaly akizungumza baada ya kuteuliwa kama mgombea wa chama cha RHDP katika uchaguzi wa urais wa Oktoba 31, 2020. Machi 12, 2020.
Amadou Gon Coulibaly akizungumza baada ya kuteuliwa kama mgombea wa chama cha RHDP katika uchaguzi wa urais wa Oktoba 31, 2020. Machi 12, 2020. REUTERS/Thierry Gouegnon
Matangazo ya kibiashara

Uteuzi wa Amadou Gon Coulibaly ambao ulikuwa ukisubiriwa kwa muda mrefu kama mgombea wa chama tawala unakuja wiki moja baada ya Alassane Ouattara kutangaza kwamba hatawania tena kwa muhula wa tatu katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Oktoba 31.

Amadou Gon Coulibaly amepitishwa kwenye nafasi hiyo katika mkutano wa kamati kuu ya chama uliofanyika Alhamisi jioni wiki hii.

Katika siku za hivi karibuni, Alassane Ouattara ameonyesha ladha yake kwa mshangao na mkakati wa upande.

Wengi hawakuamini kwamba Amadou Gon Coulibaly atapewa bahati hiyo ya kupeperusha bendera ya chama tawala cha RHDP katika uchaguzi huo wa Oktoba 31.

"Rais Houphouët alisema:" Mtaona baada yangu, kuna watu ambao katika nchi hii watafanya vizuri zaidi kuliko mimi. Na mimi acha nirejelee kauli hiyo. Nina uhakika mumechagua mtu ambaye atafanya vizuri kuliko Alassane Ouattara. Na niko tayari kushirikiana naye, " amesema Alasane Ouattara.

Nihurumieni! Acha niachie ngazi, nimechoka kwa kweli, " ameongeza Alassane Ouattara akihutubia wafuasi wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.