Pata taarifa kuu
MALI-AU-USALAMA-SIASA

Mali: Umoja wa Afrika waunga mkono Mali kufanya mazungumzo na wanajihadi

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari Februari 17, Pierre Buyoya, Mwakilishi mwandamizi wa tume ya Umoja wa Afrika nchini Mali na katika eneo la Sahel (Misahel), amezungumzia suala la mgogoro wa Mali na uwezekano wa kufanyika mazungumzo na makundi ya wanajihadi.

Rais wa zamani wa Burundi Pierre Buyoya Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika nchini Mali.
Rais wa zamani wa Burundi Pierre Buyoya Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika nchini Mali. Chatham House/Wikimedia.org
Matangazo ya kibiashara

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari Februari 18, Mwakilishi mwandamizi wa tume ya Umoja wa Afrika nchini Mali na katika eneo la Sahel (Misahel), Pierre Buyoya, amethibitisha kwamba hali ya usalama katika ukanda huo ilidorora kwa kiasi kikubwa mwaka uliopita.

Kwa kurahisisha mambo, inatakiwa "kutathmini mkakati wa utawala na usalama" kabla ya kuitia moyo Mali "kuendelea" na mazungumzo na magaidi, kwa mujibu wa Pierre Buyoya, pia rais wa zamani wa Burundi.

"Sisi Umoja wa Afrika tunaunga mkono mpango huu wa Mali wa kufanya mazungumzo na wale ambao ni viongozi wa makundi ya kigaidi. Hii ni moja ya njia za kumaliza vita. Hasa ikiwa wote ni raia wa Mali, tunawahimiza kufanya hivyo, "amesema, huku akiri kwamba ni" uamuzi ngumu ".

Kujihusisha katika mazungumzo hakuzuii matumizi ya nguvu kwa bahati mbaya. "Hivi ndivyo makundi yanayofanya mapambano ya ukombozi yanaita, fight and talk, [kupambana kivita na kuzungumza] ," amebaini Pierre Buyoya, ambaye ana imani kuwa Mali kufanya mazungumzo na magaidi itapelekea kupatikana kwa suluhisho kama nchini jirani ya Algeria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.