Pata taarifa kuu
SOMALIA-NZIGE-KENYA-ETHIOPIA

Somalia yatangaza uvamizi wa nzige kama janga la kitaifa

Nchi ya Somalia imetangaza uvamizi wa nzige katika maeneo mbalimbai ya nchi hiyo kama janga la kitaifa huku Wizara ya Kilimo, ikisema kuwa hatua hii imefikiwa baada ya wadudu hao kuendelea kuharibu mimea na sasa hali ii inatishia kuwepo kwa uhaha wa chakula nchini humo.

Hali ya uvamizi wa nzige katika eneo la Samburu nchini Kenya
Hali ya uvamizi wa nzige katika eneo la Samburu nchini Kenya Njeri Mwangii / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kuna wasiwasi kuwa, huenda ikawa vigumu kudhibiti nzige hao, kabla ya msimu wa mavuno mwezi Aprili mwaka huu.

Umoja wa Mataifa umesema, huu ndio uvamizi mkubwa wa nzige kuwahi kushuhudiwa nchini humo kwa kipindi cha miaka 25 hali ambayo pia imeathiri nchi jirani ya Ethiopia.

Somalia imekuwa nchi ya kwanza, kutangaza uvamizi huo kama janga la kitaifa, wakati huu nchi jirani ya Kenya ikikabiliwa pia na gali hii kwa mara ya kwanza baada ya miaka 70.

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Kilimo na Chakula FAO sasa linaomba msaada wa kimataifa kukubaliana na uvamizi huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.