AFRIKA KUSINI-RUSHWA-UCHUMI
Mtoto wa rais wa Afrika Kusini akiri kupokea hongo
Mtoto wa rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, Andile, amekiri kwamba alipewa kitita cha dola za Marekani Laki moja na elfu arobaini kutoka kwa kampuni inayokabiliwa na mashtaka ya rushwa.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Wadadisi wanasema tukio hilo linaweza kumvuruga baba yake kuelekea kwenye uchaguzi mkuu mwezi Mei mwaka huu.
Ramaphosa kwa sasa anakabiliwa na kibarua kigumu cha kukisafisha chama cha ANC kuhusu madai ya ufisadi kuelekea uchaguzi Mkuu tarehe nane mwezi Mei.
Kampuni ya Bosasa ambayo kwa sasa inaitwa African Global Operations inadaiwa kutowa masoko hewa ya zabuni na kusaini mikataba na serikali ambapo takriban dola milioni 120 zilipotea.