Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-DRC-JOSEPH KABILA-CENI

Rais Kabila anaondoka uongozini baada ya karibu miaka 18

Rais Joseph Kabila, baada ya kuongoza nchi yake kwa miaka 17, anatarajiwa kuondoka madarakani ifikapo katikati ya mwezi Januari mwaka 2019, lakini je, nani atachukua nafasi yake ?

Le président de la République démocratique du Congo, Joseph Kabila, s'exprimant lors d'une interview au Palais de la Nation à Kinshasa, en RDC, le 9 décembre 2018.
Le président de la République démocratique du Congo, Joseph Kabila, s'exprimant lors d'une interview au Palais de la Nation à Kinshasa, en RDC, le 9 décembre 2018. REUTERS/Benoit Nyemba
Matangazo ya kibiashara

Wagombea 17 wanawania urais, lakini ushindani mkali ni kati ya wagombea watatu, Emmanuel Ramazani Shadary, Martin Fayulu na Felix Tshisekedi.

Shadary anawakilisha muungano wa chama tawala na alichaguliwa na rais Kabila, kumrithi.

Kabla ya kuwania urais, alikuwa ni Waziri wa Mambo ya ndani na alifahamika sana kwa kuwa na msimamo mkali wa kuunga mkono maamuzi ya rais Kabila.

Hata hivyo, anakabiliwa na vikwazo kutoka kwa Umoja wa Ulaya, baada ya mwaka 2017 maandamano ya wapinzani jijini Kinshasa na kusababisha maafisa.

Martin Fayulu, yeye anawakilisha muungano wa upinzani Lamuka, anaungwa mkono na aliyekuwa Gavana wa Katanga Moise Katumbi Chapwe na makamu wa rais wa zamani Jean Pierre Bemba.

Felix Tshisekedi, mtoto wa mwanasiasa mkongwe marehemu Ettien Tshisekedi anawania chini ya chama kikuu cha upinzani UDPS, aliamua kuwania baada ya wanasiasa wa upinzani kugawanyika kuhusu mgombea mmoja, yeye na Vital Kamere walijiondoa kwenye muungano wa wanasiasa waliokuwa wamekubaliana kumuunga mkono Bwana Fayulu katika Uchaguzi huu.

Tume ya Uchaguzi inasema, mshindi atatangazwa taerehe 15 na kuapishwa tarehe 18 mwezi Januari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.