Pata taarifa kuu
SUDAN-AJALI-USALAMA

Wanafunzi zaidi ya 22 wapoteza maisha Sudan

Wanafunzi 22 wamekufa maji baada ya boti lao kuzama Jumatao wiki hii kwenye mto Nile, katika mkoa ulio kwenye umbali wa karibu kilomita 750 kaskazini mwa mji wa Khartoum, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti.

Wanafunzi wakihudhuria darasani chini ya kivuli cha mti katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Abu Shouk karibu na mji wa El Fasher, mji mkuu wa Darfur Kaskazini, Septemba 6, 2016.
Wanafunzi wakihudhuria darasani chini ya kivuli cha mti katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Abu Shouk karibu na mji wa El Fasher, mji mkuu wa Darfur Kaskazini, Septemba 6, 2016. AFP
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya watoto 40 kwa jumla walikuwa wakisafiri na boti hilo.

Wanafunzi hao walikuwa wakienda shuleni wakati wa tukio hilo, kwa mujibu wa shirika la habari la Sudan Suna, ambalo pia limeripoti kifo cha mwanamke mmoja, na watu 23 waliojeruhiwa katika tukio hilo.

Ajali kama hizi zimekua zikitokea kwenye mto Nile nchini Sudan na kusababisha raia kuwa na wasiwasi wa kusafiri kupitia mto huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.