Pata taarifa kuu
MAREKANI-SUDAN-VIKWAZO-USALAMA-UCHUMI

Marekani kuindoa Sudan kwenye orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi

Mjumbe wa Marekani nchini Sudan amesema atashirikiana na serikali ya Kahrtoum, ili kuoindoa nchi hiyo kwenye orodha ya mataifa yanayofadhili ugaidi. Steven Koutsis ameipongeza Sudan kwa kuacha kushirikiana na Korea Kaskazini katika biashara ya silaha na masuala mengine ya kijeshi.

Rais wa Sudan Omar al-Bashir, ambaye nchi yake inaendelea kukabiliwa na vikwazo vya Maekani.
Rais wa Sudan Omar al-Bashir, ambaye nchi yake inaendelea kukabiliwa na vikwazo vya Maekani. REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah
Matangazo ya kibiashara

Marekani imekuwa ikitaka Sudan kuacha ushirikiano na Korea Kaskazini iwapo inataka kuondolewa vikwazo.

Hivi karibuni rais wa Marekani Donald Trump aliamua kuongeza muda wa miezi mitatu zaidi wa makataa ya kuamua ikiwa nchi yake iondoe vikwazo dhidi ya Serikali ya Sudan au la, ikisema inahitaji muda zaidi kufanya mapitio.

Trump amesema serikali yake itafanya uamuzi huo kufikia tarehe 12 mwezi Oktoba.

Marekani inaichukulia Sudan kama nchi inayoendelea kuvunja haki za binadamu na ni moja ya nchi ambayo Marekani ilikua ikiituhumu kusaidia ugaidi duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.