Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-USALAMA

Watu 800,000 watoroka makazi yao kufuatia vurugu Ethiopia

Machafuko tangu mwezi Juni kusini mwa Ethiopia yamelazimu zaidi ya watu 800,000 kuyatoroka makaazi yao, kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa na serikali ya Ethiopia iliyotolewa Jumatano.

Vikosi vya Ethiopia vyashtumiwa  katika mauaji na unyanyasaji wa raia.
Vikosi vya Ethiopia vyashtumiwa katika mauaji na unyanyasaji wa raia. Yona Tadese/AFP
Matangazo ya kibiashara

Mapigano hayo yalitokea mnamo mwe mwaka huu, karibu kilomita 400 kusini mwa mji mkuu, Addis Ababa. Tangu wakati huo, watu zaidi ya milioni 1.2 walilazimika kuyatoroka makaazi yao.

"Vurugu zinazoendelea katika maeneo ya Gedeo na Magharibi mwa Ethiopia tangu mwanzoni mewa Juni (...) zimewalazimu watu 642,152 kuyahama makaazi yao katika eneo la Gedeo na 176,098 katika eneo la magharibi mwa 'Oromia', inasema ripoti hiyo.

Ethiopia ni nchi yenye watu milioni 100, kutoka jamii mbalimbali. Mapigano hayo yalichangia kujiuzulu manmo mwezi Februari wa Waziri Mkuu Hailemariam Desalegn.

Waziri mkuu mpya wa Ethiopia, Abiy Ahmed, ambaye aitawazwa mnamo mwezi Aprili, aliahidi kutekeleza mageuzi ya kisiasa na kiuchumi ili kuondokana na mvutano wa kikabila katika jimbo la Oromia ambako yeye hutoka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.