Pata taarifa kuu
MALI-UFARANSA-USALAMA

Askari wa Ufaransa wa kikosi cha Barkhane washambuliwa Mali

Wanajeshi wa Ufaransa wanaosaidia katika operesheni dhidi ya makundi ya kigaidi Kaskazini mwa Mali, katika doria ya pamoja na askari wa Mali wameshambuliwa nje kidogo ya mji wa Gao.

Gari la kijeshi la kikosi cha Barkhane likiteketea kwa moto baada ya shambulio la Jumapili Julai 1, karibu na Gao.
Gari la kijeshi la kikosi cha Barkhane likiteketea kwa moto baada ya shambulio la Jumapili Julai 1, karibu na Gao. © STRINGER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Haya ni mashambulizi ya pili katika muda wa siku mbili nchini Mali,dhidi ya majeshi ya yanayopambana dhidi ya makundi ya kijihadi katika eneo la Sahel baada ya shambulio siku ya Ijumaa dhidi ya makao makuu ya kikosi cha G5 Sahel huko Sevare.

Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote ya kweli kuhusiana na vifo, lakini kwenye ukurasa wake wa twitter waziri wa usalama wa Mali ameandika kuwa raia wanne wameuawa na zaidi ya ishirini kujeruhiwa na askari 4 wa kikosi cha Barkhane wako katika hali mbaya.

Kwa mujibu wa chanzo cha hospitali huko Gao, watoto walioathirika na mlipuko wa bomu ni miongoni mwa watu waliojeruhiwa.

Hata hivyo, ripoti za kijeshi hazijaeleza iwapo kuna mwanajeshi aliyepoteza maisha au kujeruhiwa.

Hili ni shambulizi linalokuja, siku mbili baada ya wanajeshi kutoka muungano wa G5 Sahel kushambuliwa katika makao makuu ya jeshi hilo huko Mali.

Ni shambulizi linalotokea wakati huu viongozi wa nchi za Afrika wakikutana katika nchi jirani ya Mauritania kujadili masuala mbalimbali likiwemo suala la Usalama.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatarajiwa kuwahotubia viongozi hao siku ya Jumatatu, na kushauriana nao namna ya kupamba ana ukosefu wa usalama katika ukanda wa Sahel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.