Pata taarifa kuu
DRC-UCHAGUZI-SIASA

Mvutano waibuka kuhusu orodha ya vyama vilivyoruhusiwa kushiriki uchaguzi DRC

Kumejitokeza hali ya sintofahamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ikiwa zimesalia siku tatu kabla ya kutangazwa wagombea katika uchaguzi wa wakuu wa mikoa mwezi Desemba mwaka huu.

Mwenyekiti wa CENI, Tume ya Uchaguzi nchini DRC, Corneille Nangaa.
Mwenyekiti wa CENI, Tume ya Uchaguzi nchini DRC, Corneille Nangaa. AFP/JOHN WESSELS
Matangazo ya kibiashara

Orodha ya vyama vya kisiasa vilivyruhusiwa kushiriki uchaguzi bado haijashughulikiwa upya na Wizara ya Mambo ya Ndani wakati ambapo orodha hiyo imeendelea kupingwa na vyama mbalimbali vya kisiasa nchini humo.

Zaidi ya vyama vya kisiasa hamsini vimewasilisha malalamiko yao, ikiwa ni pamoja na chama cha UDPS kinachoongozwa na Felix Tshisekedi. Kwa sababu orodha hii inajumuisha sio chini ya vyama vya kisiasa 4 vyenye jina moja la UDPS, vikitumia alama au nembo moja, kwa mfano UDPS, iliyoundwa kutoka chama hicho na Waziri Mkuu Bruno Tshibala. Hata hivyo, CNSA, mamlaka inayohusika na kutathmini malumbano na kuhakikisha kuna kuwepo na ubora katika mchakato wa uchaguzi, ilikua imepatia ufumbuzi suala hili zaidi ya mwezi mmoja uliopita, lakini Wizara ya Mambo ya Ndani haikuzingatia uamuzi huo na haikuweka chama hicho kwenye orodha yake.

Uamuzi uliotolewa mnamo mwezi Machi na CNSA ulikua wazi, ulikua uliomba Wizara ya Mambo ya Ndani kutambua chama cha UDPS cha Felix Tshisekedi badala ya kile kinachoongozwa na Waziri Mkuu Bruno Tshibala, na kumtaka waziri huyo mkuu kuunda chama chake chenye jina tofauti na alama au nembo tofauti na UDPS ya Bw Tshisekedi. Uamuzi wa CNSA unakwenda sambamba na makubaliano ya kisiasa yaliyofikiwa mnamo mwezi Desemba 2016, ambayo yalitaka kusikuepo na "mgawanyiko wa vyama vya siasa".

Tatizo, uamuzi huu wa CNSA haukufuatwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Kornelle Nangaa amethibitisha kwamba wagombea watasahihishwa kupitia orodha ya vyama vya siasa iliyopingwa. "Tutachukua orodha iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani kupitia gazeti la serikali (...). Hatuandai uchaguzi kulingana na makubaliano, ni kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi hii, " amesema Mwenyeiti wa Tume ya Uchaguzi (CENI) Corneiil Nangaa.

Ibara ya19 ya sheria ya uchaguzi inasema wazi kwamba "chama cha siasa hakiwezi kutumia alama au nembo iliyochaguliwa na chama kingine". Orodha ambayo tume hiyo inataka kutumia ni kinyume na sheria. Ceni ambayo inatakiwa kulingana na Katiba "kuhakikisha utaratibu wa mchakato wa uchaguzi unakwenda vizuri". Bila kusahau machafuko ambayo yanaweza kusababishwa na hali hiyo wakati wa uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.