Pata taarifa kuu
SIERRA LEON-UCHAGUZI-MATOKEO

Tume ya Uchaguzi nchini Sierra Leone kumtangaza mshindi wa urais

Tume ya uchaguzi nchini Sierra Leone imesema itahesabu upya kura kutoka vituo kadhaa vya kupigia kura na kwamba inatarajia kutangaza matokeo rasmi baadaye siku ya Jumanne.

Raia wa  Sierra Leone walivyojitokeza wiki iliyopita jijini Freetown kupiga kura
Raia wa Sierra Leone walivyojitokeza wiki iliyopita jijini Freetown kupiga kura LA Bagnetto
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa iliyotolewa usiku wa kuamkia siku ya Jumanne na tume hiyo, imesema mpaka sasa hakuna kura zilizofutwa na kwamba vituo 154 kati ya elfu 11,122 zitahesabiwa upya.

Wakati huu asilimia 75 ya kura zote zikiwa zimehesabiwa, hakuna mgombea anayeoonekana kupata ushindi wa zaidi ya asilimia 55 ili kutangazwa mshindi na kuunda serikali.

Dalili zote zinaonesha kuwa kutakuwa na duru ya pili ya Uchaguzi huo baada ya wiki mbili.

Ushindani mkali ni kati ya mgombea wa upinzani Julius Maada Bio anayeongoza kwa asilimia 43.3 akifuatiwa na mgombea wa chama tawala Samura Kamara aliyepata asilimia 42.6.

Raia wa nchi hiyo walipiga kura wiki iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.