Pata taarifa kuu
DRC-LUMBUBASHI-MTANDAO

Mashirika ya kiraia mjini Lubumbashi yafungulia mashtaka kampuni za simu

Mashirika nane ya kiraia mjini Lubumbashi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, yamekwenda Mahakamani kuyafungulia kesi kampuni nne za simu.

Biashara mjini Lubumbashi nchini DRC
Biashara mjini Lubumbashi nchini DRC www.rfi.fr
Matangazo ya kibiashara

Hubert Tshiswaka, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la kutetea haki za binadamu na utafiti mjini Lubumbashi amesema hatua ya kampuni hizo za simu, ni kinyume na haki za binadamu.

Mashirika hayo yanataka Mahakama, kuamua kuwa kwa kipindi cha miaka mitatu, hatua ya kampuni hizo kuzima mtandao na kutatiza mawasiliano, ni kinyume cha sheria.

Mwaka 2015, mji wa Lubumbashi ulikumbwa na ukosefu wa mtandao kwa siku 23, sawa na mwaka 2016, 2017 na 2018 ili kuwazuia raia kuwasiliana kwa hofu kuwa ingesababisha machafuko ya kisiasa nchini humo.

“Hii sio kawaida, kupata mtandao ni haki,” amesema Tshiswaka.

Aidha, mashirika hayo ya kiraia yanasema kuwa hatua hiyo ilichukuliwa na kampuni hizo kwa ushirikiano na serikali iliyosababisha hasara kubwa miongoni mwa wafanyibiashara na kutatiza maendeleo ya kiuchumi.

Mara ya mwisho kwa mtandao kufungwa nchini DRC, ilikuwa ni tarehe 20 mwezi huu baada ya Kanisa Katoliki kuitisha maandamano ya kumshinikiza rais Joseph Kabila kuondoka madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.