Serikali ya Burundi, inaendelea na mchakato wa kuibadilisha Katiba ili kuruhusu mgombea urais kuongoza kwa muda wa miaka saba badala ya mitano. Upinzani unalalamika kuwa, wanasiasa na wanaharakati wake wanakamatwa na kuzuiwa wanapojaribu kuwashawishi wananchi kukataa mchakato huo. Tunachambua hili.