Pata taarifa kuu
WHO

WHO yasema nusu ya walioambukizwa HIV hawajifahamu

Kuelekea kuadhimisha siku ya ukimwi duniani Desemba 1, Shirika la afya duniani WHO linasema karibu nusu ya watu walioambukizwa  virusi vya HIV ambao ni sawa watu Milioni 14 hawafahamu ikiwa wameathirika.

Nembo ya Ukimwi
Nembo ya Ukimwi DR
Matangazo ya kibiashara

Shirika hilo sasa linataka serikali mbalimbali duniani kusaidia kupatikana kwa vifaa maalum vya upimaji wa virusi hivyo, ili watu wavinunue na kujipima nyumbani.

Aidha, takwimu za WHO zinasema watu Milioni 36.7 wanaishi na virusi hivyo kote duniani.

Nchini Afrika Kusini, kliniki ya kujaribu chanjo ya virusi inayotarajiwa kuona ikiwa itasaidia kupambana na janga hili.

Tangu mwaka 1983 wakati virusi hivyo vilipogunduliwa, wanasanyansi, watafiti wa kiafya na Madaktari wamekuwa wakijaribu kutafuta tiba ya ugonjwa huu bila mafanikio.

Utafiti umeonesha kuwa vijana wengi wenye umri kati ya miaka 18 hadi 35 ndio wanaopata maambukizi ya ukimwi na serikali nchini humo imekuwa ikitoa elimu ya kupambana na maambukizi haya.

Watu walioambukizwa virusi hivi hutumia vidonge vya ARV'S kupambana na makali ya maambukizi hayo.

Maambukizi ya ukimwi yanaambukizwa kupitia ngono kati mtu aliyeambukizwa, kuongezewa damu iliyo na maambukizi  na kutumia vifaa vyenye ncha kali ambavyo mtu aliyeambukizwa ametumia.

Namna ya kujikinga na maambukizi haya ni kujiepusha na ngono, kutumia mipira lakini pia kuepuka damu iliyoathiriwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.