Pata taarifa kuu
SOMALIA - USALAMA

Majimbo mawili hasimu nchini Somalia yasitisha mapigano

Waziri mkuu nchini Somalia amesema zoezi la sitishwaji wa mapigano kati ya majimbo mawili hasimu yaliyoshuhudia mauaji ya watu 29 limefanikiwa.

Abdiweli Mohamed Ali Gaas, Raisi wa eneo lililojitenga Somalia Putland
Abdiweli Mohamed Ali Gaas, Raisi wa eneo lililojitenga Somalia Putland AFP PHOTO/STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Jimbo la Galmudug na lililojitenga la Puntland yamekuwa na historia ya mapigano ambapo hivi karibuni vikosi vyao vilikabiliana kufuatia mgogoro wa mpango wa majengo huko Galkayo,mji uliogawanyika mara mbili.

Taarifa ya ofisi ya waziri mkuu Omar Sharmake ilieleza kuwa waziri huyo alifika mjini Galkayo juma lililopita kujadiliana na kukubaliana usitishwaji wa mapigano ikiwemo na kuanzisha mazungumzo ya awali kuhusu mkataba wa amani.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa waziri Sharmake alikutana na kiongozi wa jimbo la Galmudug Abdikarim Hussein Guled na wa Putland Abdiweli Mohamed Ali na kushuhudia kutawanyika kwa wapiganaji wa pande hasimu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.