Pata taarifa kuu
CHAD-BOKO HARAM

Wanamgambo wa Kiislamu kutoka Chad wajiondoa kutoka Boko Haram

Zaidi ya wapiganaji elfu moja, raia wa Chad wamejiondoa katika kundi la Boko Haram linaloendesha harakati zake nchini Nigeria na nchi jirani, na kuamua kurejea nchini mwao, Mkuu wa mkoa Ziwa Chad (magharibi mwa Chad) amesema kwenye makala ya "Newsday" ya BBC.

Maeneo yaliyo pembezoni mwa ziwa Chad yameendelea kulengwa na mashambulizi ya Boko Haram, kama kijiji hiki cha Ngouboua, mwezi Aprili mwaka 2015.
Maeneo yaliyo pembezoni mwa ziwa Chad yameendelea kulengwa na mashambulizi ya Boko Haram, kama kijiji hiki cha Ngouboua, mwezi Aprili mwaka 2015. AFP PHOTO / PHILIPPE DESMAZES
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Dimouya Souapepe, wanamgambo hao waliojitenga na kundi la Boko Haram, wakiwemo wanawake na watoto, wamekua wakijisalimisha kwa viongozi kwa kipindi cha miezi miwili.

Wanajihadi hao wa zamani hawatawekwa jela, lakini watasikilizwa na viongozi wa Chad kabla ya kujiunga na familia zao, amesema afisa mmoja wa Chad.

Wakati huo huo, jenerali Tukur Buratai, Mkuu wa majeshi ya Nigeria, amesema kwamba 60% ya wapiganaji wa Boko Haram ni kutoka Nigeria.

Jenerali Buratai alitoa taarifa hiyo katika mkutano wa hivi karibuni mjini Maiduguri, kaskazini mashariki mwa Nigeria, akiwa pamoja na Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa katika Afrika Magharibi, Mohammed Ibn Chambas, kwa mujibu wa tovuti ya habari ya AllAfrica.

Boko Haram, kundi ambalo lilianzishwa mwaka 2002 na kiongozi wa Kiislamu kutoka Nigeria, Mohammed Yusuf, limesababisha maelfu ya vifo kaskazini mashariki mwa Nigeria, lakini pia nchini Cameroon, Niger na Chad, toka mwaka 2009 hadi sasa.

Kundi hili lilianza kupotza baadhi ya maeneo tangu mwaka 2015, kutokana na mashambulizi ya kijeshi dhidi yake yanayoendesgwa na majeshi kutoka nchi nne.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.