Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-ZUMA

Rais Zuma aondoa pingamizi mahakamani kuzuia ripoti ya mkaguzi wa mali ya uma

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, hatimaye ameondoa pingamizi lake mahakamani alilotaka kuzuiwa kuchapishwa kwa ripoti ya mkaguzi mkuu wa mali ya uma kuhusu uhusiano aliokuwa nao na familia ya Gupta.

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, 17 Machi 2016.
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, 17 Machi 2016. REUTERS/Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

Awali mawakili wa rais Zuma walitarajiwa kuishawishi mahakama kutoa agizo la kuzuiwa kuchapishwa kwa ripoti ya mwisho ya mkaguzi wa mali ya uma kuhusu shauri lililokuwa limewasilishwa na chama cha upinzani cha DA.

Wadadisi wa mambo wanaona kuwa, hatua hii ya rais Zuma kuamua kuondoa pingamizi lake mahakama, huenda ikawa imetokana na shinikizo kubwa lililowekwa dhidi yake, akitakiwa kujiuzulu nafasi yake.

Vyama vya upinzani nchini humo vikiongozwa na chama kikuu cha upinzani cha Democratic Alliance, walishirikiana na asasi nyingine za kiraia kupinga zuio la Rais Zuma.

Upinzani wenyewe unataka ripoti ya mkaguzi wa mali ya uma, Thuli Mondosela ichapishwe haraka iwezekanavyo ili kujua ukweli ikiwa kiongozi wao wa nchi alikuwa anateua mawaziri kutokana na urafisi aliokuwa nao na familia ya Gupta.

Thuli Madonsela, mkurugenzi wa ofisi ya mkaguzi wa mali ya uma aliyemaliza muda wake, 7 Juni 2016.
Thuli Madonsela, mkurugenzi wa ofisi ya mkaguzi wa mali ya uma aliyemaliza muda wake, 7 Juni 2016. REUTERS/Siphiwe Sibeko/File Photo

Siku ya Jumanne mahakama kuu ilikataa pingamizi lililowasilishwa na waziri wa ushirikiano Des van Rooyen ambaye nae alitaka kuunganishwa kwenye kesi ya kupinga ripoti hiyo kuchapishwa.

Mbuge wa zamani wa chama tawala cha ANC Vytjie Mentor na naibu waziri wa fedha Mcebisi Jonas, wanadai kuwa walipewa na kuahidiwa kazi hizo na familia ya Gupta.

Na ni kwasababu ya madai haya, ndio yalipelekea ofisi ya mkaguzi wa mali za uma, kuanzisha uchunguzi rasmi kuhusu uhusiano uliopo kati ya rais Zuma na familia hiyo, baada ya chama cha upinzani cha DA, kufungua shauri.

Maandamano makubwa yanatarajiwa kuanzia leo nje ya mahakama kuu hadi kwene mahakama ya katiba, ambapo wafuas wa upinzani, wanafunzi, asasi za kiraia na maaskofu wataungana kushinikiza rais Zuma aondoke madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.