Pata taarifa kuu
VYOMBO VY HABARI-FMM

Marie-Christine Saragosse: usalama wa waandishi wa habari ni kipaumbele

Mkurugenzi wa shirika la habari la Ufaransa la France Media Monde, Bi. Marie-Christine Saragosse, ameitolewa wito jumuiya ya kimataifa kuwalinda wanahabari wanaofanya kazi katika mazingira hatarishi kama maeneo ya vita.

Marie-Christine Saragosse, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la utangazaji la Ufaransa la FMM.
Marie-Christine Saragosse, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la utangazaji la Ufaransa la FMM. FMM
Matangazo ya kibiashara

Bi. Saragosse ambaye anaongoza vituo vya redio na televisheni vra RFI, France 24 na Monte Carlo Doualiya ameyasema hayo katika muktadha wa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya kutokomeza hali ya kutokujali uhalifu dhidi ya waandishi wa habari.
Bi. Saragosse amesema hayo katika kuwakumbuka waandishi wa habari wa Idhaa ya kifaransa ya RFI, Ghislaine Dupont na Claude Verlon, waliouawa nchini Mali mwaka 2013.

Aidha, kutokana na hatari zinazojitokeza daima, Saragosse amesema France Medias Monde imeandaa na kutekeleza mfumo wa kinga na usimamizi wa hatari zinazowakabili waandishi wa habari hasa katika maeneo ya vita.

Miongoni mwa sera hiyo ni kuwataka waandishi wa habari wafanye kazi zao na kujizuwia kuongeza yasiyo habari ambayo ni sahihi hasa maeneo ambapo demokrasia inaminywa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.