Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-MAANDAMANO

Polisi, raia waripotiwa kufa katika maandamano ya kushinikiza Rais Kabila aondoke madarakani

Polisi wawili wameripotiwa kufa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, wakati wa maandamano ya upinzani ambayo Serikali imepiga marufuku baada ya kuripoti kwa vurugu kubwa kwenye baadhi ya maeneo.

Baadhi ya vijana wakiwa wamechoma matairi kwenye moja ya barabara za Kinshasa
Baadhi ya vijana wakiwa wamechoma matairi kwenye moja ya barabara za Kinshasa https://cdn-images
Matangazo ya kibiashara

Maandamano haya ya upinzanik yaliitishwa na mwanasiasa mkongwe nchini humo na kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha UDPS, Ettiene Tshisekedi wa Mulumba, ambaye aliwataka wananchi kujitokeza kwenye maandamano ya wiki hii kuongeza shinikizo kwa utawala wa Rais Josephu Kabila.

Mbali na vifo hivi vya Polisi, waandamanajik kadhaa pia wameripotiwa kufa mjini Kinshasa na maeneo mengine ya nchi ambako maandamano haya yamefanyika.

Polisi wametumia mabomu ya machozi na risasi za mpira kuwatawanya mamia ya waandamanajik wa upinzani mjini Kinshasa, wanaotaka kuondoka madarakani kwa Rais Josephu Kabila ambaye muhula wake unatamatika mwaka huu.

Waandamanaji wa upinzani nchini DRC wakiwa kwenye barabara za jiji la Kinshasa.
Waandamanaji wa upinzani nchini DRC wakiwa kwenye barabara za jiji la Kinshasa. DR

Polisi walilazimika kutumia nguvu kukabiliana na waandamanaji mjini Kinshasa, baada ya vijana wa upinzani waliokuwa wakishiriki maandamano haya, kuanza kuwarushia mawe Polisi pamoja na kulenga vituo vyao, kati kati mwa jiji hilo.

Waandamanajik hao walikumbana na upinzani wa Polisi wakati walipojaribu kusonga mbele kwenda kwenye ofisi za bunge la kitaifa.

Moshi mkubwa umeshuhudiwa kutoka kwenye matairi, magari binafsi na daladala kwenye eneo la Limete, magharibi mwa mji wa Kinshasa, kuliko makao makuu ya chama kikuu cha upinzani cha UDPS, huku matairi mengi yakichomwa kwenye barabara maarufu ya Lumumba Boulevard.

Waandamanajik hao wakiwa na bendera zenye rangi nyeupe na blu, rangi ambazo huvaliwa sana na kiongozi wa upinzani, Etienne Tshisekedi, mwenye umri wa miaka 83, ambaye vuguvugu lake limeitisha maandamano ya nchi nzima Jumatatu ya wiki hii kushinikiza kuondoka madarakani kwa Rais Josephu Kabila, itakapofika mwezi December mwaka huu wakati muhula wake utakapo tamatika.

Polisi mjini Beni wakiwa wamemkamata mmoja wa waandamanaji hivi karibuni
Polisi mjini Beni wakiwa wamemkamata mmoja wa waandamanaji hivi karibuni REUTERS/Kenny Katombe

Rais Kabila ambaye ameongoza taifa hilo toka mwaka 2001, anazuiwa na katiba ya nchi hiyo kuwania urais kwa muhula wa tatu, lakini mpaka sasa hajaonesha ishara yoyote ya kutaka kuondoka madarakani kwa muda uliopangwa.

Kabla ya makabiliano kati ya waandamanaji na Polisi, wananchi walichoma moto bango kubwa la Rais Kabila, lililokuwa na ujumbe unaozitaka pande zinazovutana nchini humo kutafuta maridhiano yah kitaifa kupitia njia ya “mazungumzo”.
Vijana walifunga barabara ya Lumumba Boulevard, na kuwaruhusu waandishi wa habari pekee kupita.

Jiji la Kinshasa kwa sehemu kubwa sikuj ya Jumatatu lilisalia kimya, hukuj kwenyeh baadhi ya vitongoji na miji wazazi wakiacha kuwapeleka shule watoto wao kwa hofu ya kutokea vurugu, huku maduka mengi pia yakiwa yamefungwa.

Joseph Kabila, rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Februari 3, 2015.
Joseph Kabila, rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Februari 3, 2015. © AFP PHOTO / CARL DE SOUZA

Idadi kubwa ya Polisi na wanajeshi pia walionekana kupiga doria kwenye mji wa pili kwa ukubwa nchini humo wa Lubumbashi, ambapo ofisi za upinzani zilizingirwa huku maandamano yakishuhudiwa kwenye maeneo mengi ya mji huo.

Haya yanajiri wakati huu, Rais Josephu Kabila akiwa jijini New York Marekani ambako anahudhuria mkutano mkuu wa 71 wa baraza la umoja wa Mataifa, huku suala la mashariki mwa DRC, likitarajiwa kuwa ajenda ya wakuu wa dunia, huku yeye mwenyewe akisubiriwa ikiwa atatangaza mustakabali wa siasa za nchi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.