Pata taarifa kuu
AMNESTY-DRC

Amnesty International yalaani ukandamizaji dhidi ya upinzani

Shirika la kimataifa la haki za binadamU, Amnesty international limezituhumu mamlaka za jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kuhusika katika ukandamizaji dhidi ya wale wanaopinga mwenendo wa rais Joseph Kabila wa kutaka kusalia madarakani hata baada ya kutamatika kwa mihula yake miwili.

Rais wa DRC, Joseph Kabila, akiwasili katika mji mkuu wa moja wa zamani wa Katanga, Lubumbashi Juni 13, 2016.
Rais wa DRC, Joseph Kabila, akiwasili katika mji mkuu wa moja wa zamani wa Katanga, Lubumbashi Juni 13, 2016. REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti iliyochapishwa Juma hili, shirika hilo linasema viongozi wa serikali wanatumia taasisi za umma ili kuzuia kujiandaa kwa uchaguzi mkuu na kuwashughulikia wakosoaji wake.

Hata hivyo serikali imetupilia mbali tuhuma hizo. Lambert Mendeambaye ni msemaji wa serikali akiwa pia Waziri wa Habari, amesema ripoti ya shirika la kimataifa la Amnesty International ni uzushi mtupu.

Hayo yanajiri wakati Alhamisi wiki hii katika ufunguzi wa vikao vya bunge na baraza la Seneti Spika wa bunge Aubin Minaku na mwenyekiti wa baraza la seneti Kengo wa Dondo walitoa wito kwa wanasiasa waliopo kwenye mjadala wa kitaifa kuzungumza huku wakibaki kwenye muongozo wa katiba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.