Pata taarifa kuu
ZAMBIA

Joto la uchaguzi lazidi kupanda Zambia

Ikiwa zimebaki siku tatu tu kabla ya wananchi wa Zambia hawajapiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa rais, upinzani unalalamika kuhujumiwa na Serikali pamoja na tume ya uchaguzi.

RFI
RFI RFI
Matangazo ya kibiashara

Mwishoni mwa juma, tume ya uchaguzi nchini Zambia, iliomba radhi kwa vyama vya siasa baada ya kubainika kuwa ilisafirisha kwa siri masanduku ya kupigia kura kwenda kwenye vituo bila kutoa taarifa, hatua ambayo upinzani unasema ni hujuma dhidi yao.

Polisi inasema imejipanga kuhakikisha uchaguzi wa mwaka huu unafanyika kwa amani na kwamba hakuna mtu ambaye atazuiwa kwenda kupiga kura, kama alivyotoa hakikisho msemaji wa jeshi la Polisi nchini Zambia, Rae Hamoonga.

Kwa upande wa chama cha UPND kupitia katibu mkuu wake, Stephen Katuka, anasema kuwa wao wanajiepusha na vurugu ambapo wamewataka wafuasi wao pia kujiepusha na vurugu kwakuwa wana imani ya kuibuka na ushindi kwenye uchaguzi wa alhamisi ya wiki hii.

Uchaguzi wa Alhamisi ya wiki hii, unatajwa kuwa ni kipimo tosha kwa utawala wa Lungu, ambaye anakosolewa kwa kushindwa kukabili changamoto za kiuchumi toka aingie madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.