Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-PISTORIUS

Pistorius aonyesha majaji ulemavu wake kabla ya hukumu

Bingwa wa zamani wa michezo ya walemavu, Oscar Pistorius, amejaribu kuwashawishi majaji kwa kuwaonyesha ulemavu wake wakati alipokua mahakamani leo Jumatano.

Bingwa wa zamani wa michezo ya walemavu, Oscar Pistorius, akijiandaa na kutembea mahakamani bila miguu yake bandia Pretoria Juni 15, 2016.
Bingwa wa zamani wa michezo ya walemavu, Oscar Pistorius, akijiandaa na kutembea mahakamani bila miguu yake bandia Pretoria Juni 15, 2016. AFP / Sibongile KHUMALO
Matangazo ya kibiashara

Oscar Pistorius amefanya hivyo kwa ombi la mwanasheria wake, ambaye alitaka kuwashawishi majaji kwa kuwazuia kuchukua adhabu ya kifungo cha miaka kumi na tano jela kutokana na ulemavu huo.

Mbele ya kamera kutoka duniani kote ambazo zimekua zirusha kesi hiyo moja kwa moja, Oscar Pistorius, alivua miguu yake ya bandia inayomsaidia kutembea, huku akijaribu kutembea bila viato hivyo mahakamani mjini Pretoria.

Mwanasheria wake, Barry Roux, amejaribu kujitetea akisema kwamba mteja wake hana uwezo wa kujitetea, huku Bw Pistorius akiendelea kutembea mahakamani, machozi yakimtoka.

Kabla ya wakati huu mgumu kwa bingwa huyo wa zamani wa michezo ya walemavu, Wakili Roux ameiomba mahakama kutokubali kushawishiwa na picha ya uongo iliyotolewa na familia ya Reeva Steenkamp.

Hata hivyo, familia ya Reeva Steenkamp wamewahakikishia majaji kwamba Oscar Pistorius alimuua kwa maksudi binti yao baada ya mabishano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.