Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-SUDAN KUSINI

Jeshi la Ethiopia langia Sudan Kusini

Ethiopia imeanzisha operesheni ya kijeshi nchini Sudan Kusini kwa lengo la kuwaokoa watoto zaidi ya mia moja waliotekwa nyara wakati wa uvamizi wa watu wenye silaha kutoka jamii ya Murle waliotokea Sudan Kusini.

Askari wa Ethiopia.
Askari wa Ethiopia. © REUTERS/Tobin Jones/AU UN IST PHOTO
Matangazo ya kibiashara

Watu hao waliendesha shambulio katika vijiji vya Nuer nchini Ethiopia, karibu na mji wa Gambella. Shambulio liligharimu maisha ya watu zaidi ya 200 na kuzua wimbi la hasira nchini Ethiopia.

Ethiopia imethibitisha kwamba jeshi lake limeingia nchini Sudan Kusini katika kwa lengo la kuwatafuta mamia ya watoto waliotekwa nyara katika ardhi ya Ethiopia na wapiganaji kutoka jamii ya watu wa Murle. Ethiopia imesema kwamba tayari imegundua sehemu ambapo watoto hao wamefichwa na kwamba operesheni hiyo inaendeshwa kwa pamoja na serikali ya Sudan Kusini.

Juba kwa upande wake, kupitia Waziri wake wa Mambo ya Nje, imelitaka jeshi la Ethiopia kutokwenda mbali na mpaka wake. Mkuu wa majeshi wa Sudan Kusini anatarajiwa Ijumaa hii mjini Addis Ababa.

Askari wa Ethiopia kuvuka mpaka na kuingia nchini Sudani Kusini inaonyesha uamuzi wa Ethiopia kujibu shambulio hilo la Murle. serikali imetangaza siku mbili za maombolezo ya kitaifa kufuatia vifo vya watu zaidi ya 200, waliouawa katika shambulio la hivi karibuni katika vitongoji vya mji wa Gambella

Mapigano ya kikabila yamekua yakitokea mara kwa mara katika mkoa huu wa mpakani kati ya watu kutoka jamii za Murle, Nuer na Anouak, lakini katika shambulio la hivi karibuni washambuliaji walikua walibebelea bunduki za aina ya Kalashnikov huku wakivalia magwanda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.