Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-UCHUMI-FARU

Mahakama yafuta marufuku ya kuuza pembe ya faru kwenye Soko la Afrika Kusini

Mahakama Kuu ya Afrika Kusini Alhamisi hii Novemba 26 imefuta marufuku dhidi ya biashara ya ndani ya pembe faru. Marufuku iliyowekwa mwaka 2009 ili kupiga vita ujangili.

Mahakama Kuu ya Afrika Kusini yafuta marufuku kuhusu biashara ya pembe ya pembe kwenye masoko nchini humo.
Mahakama Kuu ya Afrika Kusini yafuta marufuku kuhusu biashara ya pembe ya pembe kwenye masoko nchini humo. REUTERS/Rogan Ward
Matangazo ya kibiashara

Mahakama Kuu imebaini kwamba serikali ilishindwa kufuata utaratibu wa kisheria wa maoni ya wananchi kabla ya kuweka marufuku hiyo.

Hukumu inafuata rufaa iliyowasilishwa kwenye Mahakam kuu na wafugaji wakuu wawili wa faru nchini Afrika Kusini.

Mwaka jana, Afrika Kusini ilipoteza rekodi ya faru weupe na weusi 1,215, kwa jumla ya faru zinazokadiriwa kufikia 20,000. Afrika Kusini inahifadhi 80% ya wanyama hao katika bara zima la Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.