Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-UCHAGUZI-SIASA

Côte d'Ivoire: rufaa kukataliwa, matokeo yathibitishwa

Nchini Côte d’Ivoire, Baraza la Katiba limethibitisha tena ushindi wa Alassane Ouattara kufuatia uchaguzi wa rais wa Oktoba 25. Alassane Ouattara ataapishwa Jumanne hii asubuhii katika ukumbi Ikulu ya rais mjini Abidjan. Rufaa ya Mamadou Koulibaly, ambaye alipata 0.11% ya kura katika uchaguzi huo, imekataliwa.

Mkuu wa Mahakama ya Katiba ya Côte d’Ivoire, Amadou Koné, wakati akithibitisha matokeo ya uchaguzi wa rais, Novemba 2, 2015, Abidjan.
Mkuu wa Mahakama ya Katiba ya Côte d’Ivoire, Amadou Koné, wakati akithibitisha matokeo ya uchaguzi wa rais, Novemba 2, 2015, Abidjan. REUTERS/Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Kulikuwa na rufaa nne kwa jumla kwenye meza ya Baraza la Katiba. Rufaa zote hizo ziliwasilishwa na kiongozi wa upinzani, Mamadou Koulibaly. Spika wa zamani wa Bunge la Côte d’Ivoire alishtumu hali iliyogubika uchaguzi na kudai kutothibitisha ushindi wa Alassane Ouattara katika uchaguzi wa urais.

Baraza la Katiba limefutilia mbali madai hayo, na kubaini kwamba uchaguzi ulifanyika katika mazingira mazuri, na kuchukulia madai hayo kuwa hayana msingi wowote.

Mwenyekiti wa Baraza la Katiba, Mamadou Koné, amesma : " alifuatilia matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa urais ya Oktoba 25, 2015. Ibara ya kwanza, madai ya Mamadou Koulibaly yamefutiliwa mbali. Ibara ya pili : uchaguzi wa Oktoba 25 ulifanyika katika mazingira mazuri. Ibara ya tatu : Alassane Ouattara ametangazwa kuwa msindi katika duru ya kwanza ya uchaguzi na kwa sasa ni Rais wa Jamhuri ya Côte d’Ivoire ".

Baraza la Katiba limesahihisha ushindi wa Alassane Ouattara. Jumanne hii asubuhi, ataapishwa katika ukumbi wa Ikulu ya rais mjini Abidjan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.