Pata taarifa kuu
CAMEROON-BOKO HARAM-SHAMBULIO-USALAMA

Mashambulizi mawili yatokea Kolofa

Mashambulizi mawili yametokea mapema hii Jumapili, Septemba 13, 2015 asubuhi katika mji wa Kolofata katika mkoa wa Kaskazini mwa Cameroon. Zaidi ya watu 11wameuawa, ikiwa ni pamoja na watu wawili wanokisiwa kujilipua kwa kujitoa mhanga na watu wengine kadhaa wamejeruhiwa, baadhi wakiwa katika hali mbaya.

Pamoja na ramani mkononi, Kanali Jacob Koudji, mkuu wa majeshi wa mkoa wa Far North nchini Cameroon, akiambatana na maofisa wa Chad mwezi Machi mwaka jana katika mji wa Mora.
Pamoja na ramani mkononi, Kanali Jacob Koudji, mkuu wa majeshi wa mkoa wa Far North nchini Cameroon, akiambatana na maofisa wa Chad mwezi Machi mwaka jana katika mji wa Mora. AFP PHOTO/KAYA ABBA ALI
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi haya mawili yametokea saa 1:00 Jumapili hii. Kwa mujibu wa vyanzo vya usalama viliowasiliana na RFI, wavulana wawili wwenye umri wa miaka kumi na tano inakisiwa kuwa wamejilipua katikati mwa mji wa Kolofata. Ripoti ya mwanzo imetoa idadi ya watu tisa ambao wameuawa katika mashambulizi hayo, na watu wawili wanaokisiwa kuwa walihusika na mashambulizi. Watu 21 wamejeruhiwa, ikiwa ni pamoja na watano ambao wako katika hali mbaya, na wamesafirishwa katika hospitali ya mji wa Maroua.

Mshambuliaji wa tatu, aliye kuwa akielekea kwenye mji wa Mora, amekamatwa na viongozi wa mji huo pamoja na vilipuzi aliokua navyo, kabla hajavilipua. Kwa mara nyingine tena, ni utaratibu ule ule kama katika mashambulizi ya awali yaliotokea katika eneo hilo. Ni wimbi la mashambulizi ya kujitoa mhanga, ambayo yameendelea kulikumba eneo la kaskazini mwa Cameroon kwa muda wa miezi mitatu na mashambulizi mawili ya kujitoa mhanga yaliyotokea katika mji wa Fotokol mwezi Julai mwaka huu.

Wakati huo ilikua tukio la kwanza la aina yake nchini Cameroon. TWashambuliaji tisa waliojitoa mhanga, ikiwa ni pamoja na wasichana, walijilipua wakati huo, na kuwaua zaidi ya watu mia moja. Wakati huo kundi la Boko Haram lilinyooshewa kidole cha lawama, lakini hakuna kundi hata moja lililokiri rasmi kuhusika na mashambulizi hayo. Katika muda wa siku kumi, hii ni mara ya pili Kolofata inashambuliwa. Ni mji ulio mpakani na Nigeria, ulio karibu na msitu wa Sambisa, kilomita 130 kutoka Maiduguri, nchini Nigeria. Ngome za kihistoria za waasi wa kiislam.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.