Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-USALAMA

Gari la Boko Haram mikononi mwa jeshi la Nigeria

Jeshi la Nigeria limesema limewafanikiwa kulikamata gari linaloaminiwa kuwa la kundi la kigaidi la Boko Haram lililokuwa likisafirisha dawa za kulevya na Petroli.

Askari wakiwakamata watu 59 wa kundi la Boko Haram kutoka makambi ya kundi hilo katika jimbo la Maiduguri, Borno, kaskazini mashariki mwaNigeria, Julai 30, 2015.
Askari wakiwakamata watu 59 wa kundi la Boko Haram kutoka makambi ya kundi hilo katika jimbo la Maiduguri, Borno, kaskazini mashariki mwaNigeria, Julai 30, 2015. (AFP Photo via yahoo
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja baada ya wanajeshi Kaskazini mwa nchi hiyo kutakiwa kuyachunguza magari yote yanayopita katika ngome za Boko Haram.

Taarifa za jeshi zinasema kuwa pamoja na kulikamata gari hilo, wamekamatwa pia waliokuwa wakisafirisha dawa hizo, lakini haijafamika ni watu wangapi waliokamatwa.

Inaelezwa kuwa gari hilo limekamatwa kati ya mji wa Depchi na Geidam katika jimbo la Yobe.

Jeshi limesisitiza kuwa kukamatwa kwa dawa hizo kunadhibitsiha kuwa kundi la Boko Haram halina mpango wa kuhakikisha kuwa Kaskazini mwa Nigeria linasalia eneo la Kiislamu kwa sababu Uislamu hauruhusu matumizi ya dawa za kulevya.

Nigeria pamoja na nchi jirani imeendelea kupambana na kundi hilo ambalo tangu mwaka 2009 limesababisha zaidi ya watu elfu 15 kupoteza maisha na zaidi ya Milioni 2 kukimba kuyahama makaazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.