Pata taarifa kuu
NIGERIA-UN-MAADHIMMISHO-USALAMA

Nigeria: Ban Ki-moon ahudhuria maadhimisho ya shambulio dhidi ya jengo la UN

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameweka shahada la maua katika jengo la Umoja wa Mataifa jijini Abuja lililoshambuliwa na wanamgambo wa Boko Haram miaka minne iliyopita.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akiwasili mjini Abuja, Nigeria, Agosti 23, 2015.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akiwasili mjini Abuja, Nigeria, Agosti 23, 2015. REUTERS/Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Watu zaidi ya 20 waliuawa na mamia kujeruhiwa wakati wa shambulizi hilo na Ban Ki-moon amesema dunia itaendelea kuwakumbuka waoliangamia na wale waliojeruhiwa katika mashambulizi hayo.

Moon ambaye alianza ziara yake ya siku mbili nchini Nigeria Jumapili Agosti 23 amekutana pia na rais Muhamadu Buhari kuhusu namna ya kulishinda kundi la Boko Haram linaloendeleza mashambuluzi nchini humo na katika nchi jirani.

Hayo yakijiri mkuu wa mjeshi ya Nigeria, jenerali Tukur Buratai, aliponea kuawa katika shambulizi la kuvizia lililoendeshwa Jumamosi Agosti 22 na kundi la Islamic State Afrika Magharibi (kundi la zamani la Boko Haram). Shambulio hilo lilitokea siku moja kabla ya zaiara ya katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ban Ki-moon mjini Abuja, nchini Nigeria, ili kuadhimisha kumbukumbu ya shambulio la Boko Haram dhidi ya jengo la Umoja wa mataifa nchini humo mwaka 2011, ambalo liligharimu maisha ya watu 21.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.