Pata taarifa kuu
UFARANSA-CAMEROON-DIPLOMASIA

Nchini Cameroon, François Hollande avunja mwiko

François Hollande amekamilisha ziara yake barani Afrika kwa kuitembelea Cameroon siku ya Ijumaa wiki hii. Hii ni ziara ya kwanza ya rais wa Ufaransa nchini Cameroon tangu mwaka 1999. Rais wa Ufaransa alikutana na mwenzake Paul Biya. Pamoja, walizungumzia masuala nyeti, ikiwa ni pamoja na vita dhidi ya kundi la waasi la UPC.

François Hollande na mwenzake Paul Biya wakati wa mkutano wao Ijumaa, Julai 3, katika mji wa Yaoundé.
François Hollande na mwenzake Paul Biya wakati wa mkutano wao Ijumaa, Julai 3, katika mji wa Yaoundé. AFP PHOTO / ALAIN JOCARD
Matangazo ya kibiashara

"Nilitaka kuja hapa nchini Cameroon. Ni karibu miaka kumi na tano rais wa Jamhuri ya Ufaransa alikua hajaifanya ziara rasmi katika nchi yako Bwana rais. Nimetaka pia kuja nchini hapa kwa sababu kuna mahusiano ya binadamu kati ya nchi zetu mbili. Baadhi ya mahusiano haya yanaingia katika undani wa historia yetu. yanaweza kuwa machungu na Ufaransa bado inangalia kwa makini zama zake za zamani ili kujiandaa vizuri kwa siku zijazo nandivyo tulivyofanya", amesema François Hollande.

Katika mkutano na vyombo vya habari Ijumaa jioni, François Hollande amezungumzia hasa kumbukumbu ya machungu ya mahusiano kati ya Ufaransa na Cameroon.

" Ni kweli kwamba kulikuwa na matukio ya kutisha katika historia. Kulikuwa na ukandamizaji katika eneo la Sanaga-Maritime katika nchi ya Bamiléké na nataka nyaraka zifunguliwe kwa wanahistoria ", alisema François Hollande.

Kumbukumbu ya matukio ya kutisha ya mwaka 1950 na 1960 wakati maelfu ya wanaharakati wa uhuru waliokua wakiuounga mkono UPC waliuawa kwanza na jeshi la Ufaransa, kisha baada ya 1960 wakauawa pia na jeshi changa la Cameroon lililokua likipewa mafunzo na maafisa wa Ufaransa.

Kauli hii ni mara ya kwanza kutolewa na rais wa Ufaransa kuhusu tukio huli la kihistoriakati ya Ufaransa na Cameroon. Kamwe hakuna rais wa Ufaransa aliyejieleza kuhusu jeraha hili kubwa katika historia ya mataifa yote mawili. Hili ni tukio la kihistoria na mwikoambao umevunjwa sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.