Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-MASHAMBULIZI-USALAMA

Nigeria: watu 150 wauawa katika shambulio la Boko Haram

Kundi la Boko Haram linasadikiwa kuendesha shambulio katika kijiji cha Kukawa pembozoni mwa ziwa Chad, Kaskazini Mashariki mwa Nigeria na kuwaua takriban watu 150.

Aboubakar Shekau, kiongozi wa kundi la Boko Haram.
Aboubakar Shekau, kiongozi wa kundi la Boko Haram. Fuente: YouTube
Matangazo ya kibiashara

Wanamgambo hao wameshambulia watu waliyokua wakiswali katika Miskiti mbalimbali ya kijiji hicho, kwa mujibu wa mashahidi.

Mauaji haya mapya yanasadikiwa kutekelezwa na Boko Haram. Watu wanaokadiriwa kufikia mia moja waliuawa katika shambulio hilo lililotekelezwa na watu wanaoshukiwa kuwa wa kundi la Boko Haram katika kijiji cha Kukawa, karibu na Ziwa Chad kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Shambulio hili limetekelezwa Jumatano jioni wiki hii, wakati zaidi ya watu hamsini wenye silaha wanaoshukiwa kuwa wa kundi hilo walipowafyatulia risasi waumini wa kiislamu katika Misikiti ya kijiji cha Kukawa, muda mfupi baada ya kumalizika kwa siku ya 14 ya mwezi mtukufu wa Ramadhan.

" Ninakuhakikishieni kwamba washambuliaji waliwaua zaidi ya watu 97 ", amesema shahidi mmoja anayejulikana kwa jina maarufu Kolo, ambaye amethibitisha kuwa alihesabu miili ya watu waliouawa. Kwantami Amodu, mvuvi wa kijiji hicho, pia amethibitisha kuwa alihesabiwa zaidi ya miili 120 .

" Walizingira misikiti minne na kisha kuanza kufyatulia risasi "

Kwa mujibu wa shahidi wa tatu, Babami Alhaji Kolo, " magaidi walianza kwanza kuwachukua waumini wa kiislamu waliokua wakiswali katika Misikiti mingi. Kisha wakazingira Misikiti minne tofauti ya kijiji cha Kukawa na kuanza kuwafyatulia risasi waumini, hasa vijana na watoto ", ameongeza Alhaji Kolo.

" Baadhi ya magaidi walibakia wakichoma moto maiti, na wengine walijielekeza katika kila nyumba na kuanza kufyatua hovyo risasi wakielekeza bunduki zao kwa wanawake ambao walikuwa wakiandaa chakula cha usiku", ameendelea kusema shahidi huyo.

Boko Haram imekua ni tishio katika Ukanda wa Afrika Magharibi na Kati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.