Pata taarifa kuu
MISRI-SOKA-SHERIA

Mashabiki 11 wahukumiwa adhabu ya kifo Misri

Mahakama ya Misri Jumanne wiki hii imethibitisha hukumu ya kifo iliyotolewa dhidi ya mashabiki 11 kufuatia makabiliano yaliyosababisha vifo vya watu 74 katika uwanja wa mpira baada ya mechi ya mpira wa miguu iliyochezwa mwezi Februari mwaka 2012 katika mji wa Port Said.

Mashabiki wa Soka nchini Misri wakibeba jeneza la kijana aliyeuawa wakati wa makabiliano kati ya vikosi vya Misri na mashabiki wa klabu ya Al-Masry, katika mji wa Port-Saïd.
Mashabiki wa Soka nchini Misri wakibeba jeneza la kijana aliyeuawa wakati wa makabiliano kati ya vikosi vya Misri na mashabiki wa klabu ya Al-Masry, katika mji wa Port-Saïd. REUTERS/
Matangazo ya kibiashara

Vurugu hizo zilitokea wakati wa mechi ya ligi kuu, ambapo klabu ya Port Said, Al-Masry ilipata ushindi, dhidi ya nyota za Cairo Al-Ahly.

Hukumu ya kifo iiliyotolewa tarehe 19 Aprili, ilithibitishwa na Mahakama ya Cairo baada ya maoni yaliyotolewa na Mufti wa Misri.

Watu arobaini miongoni mwa watuhumiwa 72 walihukumiwa kifungo kiliyokati ya mwaka mmoja na miaka 15 jela. Kati yao, maafisa wawili wa klabu ya Al-Masry walihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela, vilevile maafisa wawili wa polisi waliotuhumiwa kuwawezesha mashabiki wenye silaha kuingia na kuwaacha washambuliye mashabiki wa klabu nyingine, wamehukumiwa miaka mitano jela.

Watuhumiwa wengine 21 ikiwa ni pamoja na na maafiisa wa polisi saba wameachiliwa huru

Makabiliano yaliyotokea katika mji wa Port-Saïd (kaskazini mashariki) mwa Misri ni tukio ambalo liligharimu vifo vya watu wengi nchini Misri katika nyanja ya michuano ya soka.

Vijana " wenye msimamo mkali " walishiriki kikamilifu katika ukombozi huo uliyomtimua madarakani rais Hosni Mubarak mapema mwaka 2011. Maandamano hayo yaliendeshwa katika hali ya kupinga dhidi ya machafuko yaliyotekelezwa na askari polisi.

Tangu wakati huo polisi imekua ikishtumiwa kuwa haikuingilia kati kwa makusudi wakati wa makabiliano hayo kati ya mashabiki wa timu mbili tofauti.

Hata hivyo familia za watuhumiwa waliohukumiwa adhabu ya kifo wamelani uamzi huo wa Mahakama, wakibaini kwamba rushwa imetawala katika vyombo hivyo vya seria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.