Pata taarifa kuu
AMNESTY INTERNATIONAL-NIGERIA-ICC-BOKO HARAM

Amnesty International yanyooshea kidole jeshi la Nigeria

Shirika la kimataifa linalo tetea haki za binadamu la Amnesty International limetoa wito kwa mahakama ya kimataifa ya Uhalifu wa kivita ya ICC kuanzisha uchunguzi dhidi ya viongozi wakuu wa jeshi la Nigeria wanaohusika na vitendo vya uhalifu wa kivita dhidi ya kundi la Boko Haram.

Jeshi la Nigeria laendesha mashambulizi ya anga dhidi ya Boko Haram.
Jeshi la Nigeria laendesha mashambulizi ya anga dhidi ya Boko Haram. Ben Shemang / RFI
Matangazo ya kibiashara

Amnesty International yenye makao yake makuu jijini London nchini Uingereza, imesema katika ripoti yake kwamba ina ushahidi wa kutosha unaowahusisha wanajeshi wa Nigeria katika mauaji na vitendo mbalimbali viovu.

Hata hivyo msemaji wa jeshi la Nigeria Chris Olukolade katika taarifa yake amelituhumu shirika hilo la Amnesty International na kutupilia mbali tuhuma zote dhidi ya vikosi vya jeshi serikali na kueleza kwamba hakuna ushahidi wowote kuhusu tuhuma hizi.

Upande wake rais wa Nigeria Muhammadu Buhari kupitia msemaji wake Shehu Garba, amesema atajadiliana na viongozi husika kuhusu ripoti hiyo yenye kurasa 133, na kwamba serikali ya Nigeria itafanya kila jitihada kuhakikisha utawala wa kisheria unastawi na kushughulikia kashfa zote za uvunjifu wa haki za binadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.