Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-SIASA-UCHAGUZI

Muafrika mweusi aongoza chama chenye wazungu wengi

Chama cha Upinzani cha Democratic Alliance (DA) nchini Afrika kusini kimemchagua kwa mara ya kwanza kijana na mtu mweusi kukiongoza baada ya mwenyekiti wake Bi. Helen Zille kuachia ngazi.

Mmusi Maimane, kiongozi mpya wa chama cha upinzani cha DA.
Mmusi Maimane, kiongozi mpya wa chama cha upinzani cha DA. com/mmusimaimaneforjohannesburg
Matangazo ya kibiashara

Mmusi Maimane, muhubiri katika kanisa la kiinjili na maarufu kwa jina la Obama wa Soweto mwenye umri wa miaka 34 ndiye atakayekiongoza chama hicho chenye wanachama wengi wazungu.

Katika uchaguzi uliopita, chama hicho kimeshinda kwa asilimia 22 ya kura ambayo ni mafanikio ya kihistoria ambayo tija yake haijawa ya kukisababishia wasiwasi chama cha ANC kilichopo madarakani kwa miaka ishirini nchini Afrika Kusini.

Mmsi Maimane alizaliwa na kukulia katika mji mkubwa wa Johannesburg, akiwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi, wakati familia yake ikiwa katika chama cha ANC na baadaye mwaka 2009 kujiunga na chama cha Democratic Alliance.

Kisiasa, Mmusi Maimane amejijengea umaarufu katika kumpinga Rais Jacob Zuma mara baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa rais Thabo Mbeki na kuongoza orodha ya chama chake katika uchaguzi wa serikali za mitaa mjini Johannesburg mwaka 2011 na mwaka jana katika mkoa wa Gauteng.

Baada ya uchaguzi uliopita hadi sasa, Mmusi Maimane ni kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni ambapo ni maarufu kwa kuahidi kuiongoza serikali ya Afrika kusini baada ya uchaguzi ujao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.