Pata taarifa kuu
UFARANSA-MISRI-MAUZO-UCHUMI-USALAMA

Ufaransa na Misri zatiliana saini

Ufaransa na Misri  zinatarajiwa Jumatatu wiki hii kutiliana saini kwenye makubaliano ya mabilioni ya Yuro kwa mauzo ya ndege za kivita aina ya rafale licha ya wasiwasi ulioibuliwa na watetezi wa haki za binadamu.

Ndege aina ya Rafale ikipaa juu ya piramidi mbili nchini Misri.
Ndege aina ya Rafale ikipaa juu ya piramidi mbili nchini Misri. Dassault Aviation - Fr. Robineau
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa ulinzi wa ufaransa Jean-Yves Le Drian alitazamiwa kwenda Cairo hii leo kutia sahihi mkataba wa yuro bilioni 5.2 kwa ajili ya ununuzi wa ndege 24 za kivita aina ya rafale.

Raisi wa Ufaransa Francois Hollande ameeleza kuwa mkataba huo ulipitiwa katika kipindi cha miezi mitatu ya mazungumzo ikizingatiwa kwamba kwa cairo ni hatu ay amuhimu hasa kipindi hiki cha tishio l ausalama nchini humo.

Vyombo vya habari vya Ufaransa vimekua vikizungumzia suala hilo la mauzo ya ndege kwa siku kadhaa. Rais François Hollande, alithibitisha katika tangazo alilotoa Alhamisi wiki hii iliyopita: makubaliano yalifikiwa na Misri kwa mauzo ya ndege 24 za kivita aina ya Rafale, vifaa vinavyohusiana na ndege hizo pamoja na makombora.

Mapema Alhamisi wiki hii, rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sissi alikubali makubaliano hayo na kuruhusu kusafirishwa kwa ndege hizo hadi Misri, hivyo kuhitimisha mkataba wa kiasi chaYuro bilioni 5.2 ambapo Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian anatazamiwa kuwasili Misri kutiliana saini kwa niaba ya Ufaransa na rais wa Misri kwenye mkataba wa mauzo hayo.

Mwanzoni mwa wiki iliyopita, Sheikh Mohamed ben Zayed al-Nahyan, alipokelewa katika Ikulu ya Elysée, ambapo suala la mauzo ya ndege hizo lilizungumziwa. Falme za Kiarabu zimejikubalisha kutoa pesa hizo za mauzo ya ndege za kivita kwa nchi ya Misri.

Serikali ya Misri inahitaji ndege hizo haraka iwezekanavyo. Hata hivyo Ufaransa imekubali kusafirisha ndege kadhaa kwa minajili ya uzinduzi wa upanuzi wa eneo la Suez uliyopangwa kufanyika katika majira ya joto mwaka 2015.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.