Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI

Baraza la mawaziri Sudani Kusini laahirisha uchaguzi

Baraza la mawaziri nchini Sudan Kusini siku ya Ijumaa limeahirisha uchaguzi nakuongeza muda wa rais Salva Kiir kusalia madarakani kwa miaka miwili,hatua ambayo inaonekana kudidimiza mkataba wa amani wenye lengo la kukomesha miezi 14 ya vita. 

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa habari Michael Makuei ameiambia AFP baada ya uamuzi huo chukuliwa na baraza la mawaziri kuahirisha uchaguzi hadi Julai 9, 2017 kuwa wamepitisha azimio la kuongeza muda wa utawala wa rais na bunge, ikiwa ni pamoja nafasi zote za viongozi waliochaguliwa.

Hatua hiyo inakwenda kinyume na mpango ulioafikiwa kati ya rais Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar mapema mwezi huu, ambapo walikubaliana kuanzisha serikali ya mpito ya umoja wa kitaifa katika taifa hilo lililogawanyika ambayo itadumu kwa muda wa miezi 30 kuanzia Julai 9.

Pamoja na makubaliano ya kusitisha mapigano hivi karibuni, wanadiplomasia wanasema kuwa mtafaruku unaongezeka ambapo hakuna upande wowote unaochukulia kwa dhati juhudi za kueta amani ili kumaliza vita ambayo imesababisha makumi kwa maelfu ya watu kuuawa.

Umoja wa Mataifa unaonya kuwa watu milioni mbili na laki tano wanakabiliwa na janga la njaa nchini humo.

Mapigano makali yalizuka nchini Sudani Kusini mwezi Disemba mwaka 2013 wakati rais Salva Kiir alipo mshutumu aliyekuwa makamu wake Riek Machar kwa kufanya jaribio la kumpindua jambo lililosababisha mauaji ya kutisha nchini humo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.