Pata taarifa kuu
BURUNDI-RPA-SIASA-SHERIA

Bob Rugurika aendelea kuzuiliwa jela

Nchini Burundi, ni wiki moja sasa tangu mwanahabari akiwa pia mkurugenzi wa redio RPA, Bob Rugurika, akizuiliwa jela.

Makao makuu ya radio RPA inaongozwa na mwandishi wa habari anayezuiliwa jela, Bob Rugurika, Burundi.
Makao makuu ya radio RPA inaongozwa na mwandishi wa habari anayezuiliwa jela, Bob Rugurika, Burundi. http: //www.rpa-burundi.org/
Matangazo ya kibiashara

Mkurugenzi wa radio RPA, ambayo inasikilizwa na raia wengi nchini Burundi na nchi jirani anatuhumiwa kula njama katika mauaji ya watawa watatu, raia wa Italia, waliouawa Semptemba mwaka 2014, wilayani Kamenge, kaskazini mashariki mwa mji wa Bujumbura.

Vyombo vya sheria nchini Burundi vinamtuhumu kurusha hewani mfululizo wahabari kufuatia uchunguzi redio yake iliyofanya kuhusu mauaji ya watawa watatu, baada ya mmoja kati ya watu washukiwa kuhusika na mauaji hayo, kukiri kuwa aliiagizwa na Idara ya Ujasusi ya Burundi.

Wanahabari wetu walikuatana na Bob Rugurika Jumatano Januari 28 mwaka 2015 katika jela la mkoa wa Muramvya, anakozuiliwa.

Mkurugenzi wa redio RPA, Bob Rugurika, alikamatwa siku tisa zilizopita. Baada ya kulala usiku mmoja katika jela kuu la Mpimba mjini Bujumbura, alihamishiwa Muramvya, kilomita 50 mashariki ya mji mkuu wa Burundi, Bujumbura, katika mazingira ya kutatanisha.

Kabla ya kupelekwa katika jela la mkoani Muramvya, mkurugenzi wa jela kuu la Mpimba, alimwambia Bob Rugurika kwamba anaitishwa na mwendesha mashitaka, lakini mkurugenzi wa redio RPA aliamini kuwa anapelekwa kuuawa kama inavyotokea mara kwa mara kwa baadhi ya wafungwa, wakati alipoona gari iliyokua ikimsafirisha inatumia barabara inayoelekea mikoani.

Kinachofahamika tu ni kwamba mashirika mengi yanayotetea haki za binadamu nchini Burundi, yamekua yakielezea kusononeshwa na vitendo vya kuwaua kwa wafungwa au watu wanaoshikiliwa na taasisi mbalimbali za uongozi wa nchi.

Bob Rugurika amekua harahisishiwi kwenda kujisaidia wakati alipoingizwa kwa mara ya kwanza katika jela kuu la Mpimba aidha jela la mkoa wa Muramvya. Alikua akipewa ruhusa ya kwenda kujisaidia mara tatu kwa siku, saa 12 asubuhi , saa 6 mchana na saa 12 jioni, amesema Bob Rugurika. Na iwapo atasikia haja ya kwenda kujisaidia, askari wa magereza wamekua wakimfahamisha asubiri hadi muda aliyopewa kwenda kujisaidia au ajisaidie anakolala.

Hata hivyo katika jela la Muramvya, kwa sasa Bob Rugurika amesema ameanza kupewa nafasi ya kuonana na ndugu jamaa na marafiki zake, na amebaini kwamba afya yake inaendela vizuri.

Bob Rugurika amesema uchunguzi redio yake iliyofanya umewakwaza baadhi ya viongozi wa nchi pamoja na viongozi wa juu katika ngazi zote husika. Lakini amesema ataendelea kupambana na hali hio, wala hawezi kukata tamaa.

Vyama vya wanahabari, mashirika ya kiraia, Baadhi ya Wabunge na Maseneta pamoja na raia wa kawaida wamekua wakimtembelea Bob Rugurika katika jela la Muramvya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.