Pata taarifa kuu
UTURUKI-SOMALIA-DIPLOMASIA

Pamoja na mashambulizi, Erdogan atazamiwa kuwasili Somalia

Raia 7 wa Somalia wameuawa mjini Mogadiscio katika shambulio la bomu lililokua limetegwa ndani ya gari.

Shambulizi dhidi ya hoteli ulikofikia ujumbe wa Uturuki, shambulio ambalo limegharimu maisha ya watu 5 Januari 22 mwaka 2015.
Shambulizi dhidi ya hoteli ulikofikia ujumbe wa Uturuki, shambulio ambalo limegharimu maisha ya watu 5 Januari 22 mwaka 2015. REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Wanamgambo wa Al Shabab wamekiri kutekeleza shambulio hilo, ambalo limekua limelenga hoteli walikofikia ujumbe wa Utruki, ambao umekua ukiandaa ziara ya rais wa Uturuki Erdogan nchini Somalia.

Mpaka sasa Ankara haijaahirisha ziara hio fupi. Tangu mwaka 2011, uhusiano kati ta Ankara na Mogadiscio umeendela kukua.

Rais wa Uturuki Recep Tayyit Erdogan, ambaye anakamilisha ziara yake nchi Ethiopia, amesema hatiwi wasiwasi na shambulio hilo, na amehakikisha kuwa ataendelea na ziara yake hadi nchini Somalia. Rais huyo anatazamiwa kuwasili leo Ijumaa Januari 23 mjini Mogadiscio. Kama alivyobanisha Waziri mmoja wa Uturuki, “ hali ni ya kutisha lakini Uturuki imeamua kutositisha ziara ya rais”.

Uhusiano huo kati ya Uturuki na Somalia ulianza mwaka 2011 wakati, ukame uliposhambulia mamilioni ya raia wa Somalia.

Uturuki imekua ikitoa misaada mbalimbali ya kibinadamu na imekua ikisaidi raia wa Somalia katika matukio mbalimbali. Rais Erdogan anashirikiana na mkewe katika ziara hio nchini Somalia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.