Pata taarifa kuu
KENYA-MGOMO-ELIMU

Waalim wasitisha mgomo Kenya

Nchini Kenya waalim wamechukua uamzi wa kurejea shuleni leo Jumatatu baada ya kuitikia mgomo ulioitishwa na vyama vya waalim, mgomo ambao umedumu wiki mbili. Wazazi wa wanafunzi na mashirika yanayotetea haki za watoto na wanafunzi yamepongeza hatua hiyo ya waalim.

Mji mkuu wa Kenya wa Kenya Nairobi, ambapo waalimu wanataraji kurejea shuleni, baada ya mgomo uliyodumu wiki mbili.
Mji mkuu wa Kenya wa Kenya Nairobi, ambapo waalimu wanataraji kurejea shuleni, baada ya mgomo uliyodumu wiki mbili. AFP PHOTO / SIMON MAINA
Matangazo ya kibiashara

Mgomo huo uliitishwa na chama cha Umoja wa Waalimu KNUT pamoja na KUPPET tangu mwanzoni mwa mwaka wa shule, wiki mbii zilizopita, ambapo viongozi vyama hivyo vya waalim waliwataka wanachama wao kutoripoti kazini kuanzia siku ya Jumatatu ya tarahe 5 Januari mwaka 2015.

Chama cha wazazi nchini Kenya kilikua kimewasilisha kesi mahakamani kutaka kuzuiwa mgomo huo, uamuzi uliotangazwa na katibu mkuu wake, Musau Ndunda, ambaye amesisitiza kutofumbia macho mgomo huu.

Awali katibu mkuu wa KUPET, Akelo Missori, alitupilia mbali madai ya chama cha wazazi na kuongeza kuwa hawatishwi na amri iliyotolewa na Mahakama kuwataka kusitisha kwa muda mgomo walioanzisha.

Siku moja tu baada ya mgomo huo kuanza serikali ilianzisha mazungumzo na vyama vya waalim ili kujaribu kumaliza mgomo huo nchini Kenya, bila mafanikio. Chama cha waalimu wa sekondari kimekua kikiidai serikali kiasi cha shilingi za kenya bilioni 47, lakini srikali ya Kenya ilikua ilikataa kutoa pesa hizo.

Awali serikali ilibaini kwamba ilikua ilitoa kiasi cha shilingi bilioni 9.3 kama posho kwa waalimu hao, kiasi ambacho kilipingwa na viongozi wa Kuppet hali iliyofanya mazungumzo kati yao na serikali kukwama kama ilivyotokea siku ya Jumanne Januari 6 mwaka 2015 kwa waalimu wa shule za msingi.

Waziri wa kazi nchini Kenya, Kazungu Kambi alikua alisitiza kuwa serikali haina fedha za ziada kutimiza madai ya walimu na kwamba iwapo watatekeleza madai hayo sekta nyingine zitaathirika kiuchumi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.