Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-SIASA-Sheria

Zida apania kuzindua kesi ya Sankara

Waziri mkuu wa mpito wa Burkina Faso Yacouba Isaac Zida ametangaza kuwa yuko tayari kuzindua kesi ya aliyekuwa rais wa Burkina Faso Thoma Sankara aliyeuawa mwaka 1987 katika mazingira ya kutatanisha baada ya kupinduliwa madarakani.

Waziri mkuu akiwa pia waziri wa ulinzi, luteni kanali Isaac Zida, Novemba 21 mwaka 2014.
Waziri mkuu akiwa pia waziri wa ulinzi, luteni kanali Isaac Zida, Novemba 21 mwaka 2014. REUTERS/Joe Penney
Matangazo ya kibiashara

Waziri mkuu huyo wa mpito amebaini kwamba yuko mbioni kuomba Morocco kuwa tayari kumrejesha Burkina Faso aliyekuwa rais wa nchi hiyo Blaise Compaoré iwapo vyombo vya sheria vya Burkina Faso vitamuhitaji katika kesi hiyo.

Katika mkutano na vyombo vya habari nchini Burkina Faso, Yacouba Isaac Zida ameeleza kwa muda wa saa moja na nusu majukumu yake na kazi kubwa inayosubiriwa kutekelezwa na serikali yake.

Kuhusu sekta ya sheria, Isaac Zida amesema kesi zote ambazo ziliwekwa kando katika utawala wa Blaise Compaoré zitazinduliwa, na watu watakaotajwa katika kesi hizo watafikishwa mbele ya vyombo vya sheria

Amesema hatua ya kwanza itakayochukuliwa ni kuzindua kesi ya aliyekuwa rais wa Burkina Faso Thoma Sankara. “ Watuhumiwa watafikishwa mbele ya vyombo vya sheria wasikilizwe, na iwapo watapatikana na hatia wataadhibiwa kwa mujibu wa sheria”, amesema Isaac Zida, huku akibaini kwamba hata kesi ya mwaandishi wa habari Norbery Zongo itazinduliwa.

Itakumbukwa kwamba Thoma Sankara aliuawa wakati wa mapinduzi yaliyomuweka madarakani Blaise Compaoré, Oktoba 15 mwaka 1987. Tangu wakati huo ilikua vigumu kufuatilia kesi ya mauaji ya rais Thoma Sankara, kutokana na kuwa wengi miongoni mwa waliohusika na mauaji hayo walikua katika utawala wa Blaise Compaoré.

Itafahamika kwamba hivi karibuni, rais wa mpito wa Burkina faso Michel Kafando alitangaza kwamba kaburi linaloshukiwa kuwa alizikwa Thoma sankara katika eneo la Dagnoen, mashariki mwa mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou, huenda likafukuliwa ili kufanya vipimo vya mifupa, na kujua iwapo muili wa aliyezikwa katika kaburi hilo ni wa Thoma Sankara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.