Pata taarifa kuu
DRC-UINGEREZA-POLISI-USALAMA-HAKI ZA BINADAMU

DRC: Uingereza yasitisha misaada yake kwa polisi

Serikali ya Uingereza imetangaza kusitisha misaada yake kwa ajili ya mageuzi ya jeshi la polisi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Polisi ya Congo ikiendesha operesheni "Likofi" katika mji wa Kinshasa.
Polisi ya Congo ikiendesha operesheni "Likofi" katika mji wa Kinshasa. Naashon Zalk/Bloomberg via Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Uingereza imechukua uamzi huo baada ya ripoti ya Shirika la kimataifa la haki za binadamu la Human Rights Watch kubaini vitendo vya mauaji ya kikatili na ukandamizaji vilivyotekelezwa na jeshi hilo katika Operesheni iliyojulikana kwa jina la “Likofi” mjini Kinshasa.

Askari polisi katika ambao wamejificha nyuso wakishiriki katika operesheni " Likofi" mjini Knshasa..
Askari polisi katika ambao wamejificha nyuso wakishiriki katika operesheni " Likofi" mjini Knshasa.. RFI/Habibou Bangré

Usitishwaji wa programu hiyo ya misaada unakuja baada ya ripoti ya Umoja wa Mataifa ya mwezi Oktoba mwaka 2014na ya Shirika la HRW ya hivi karibuni ambapo watu wasiopungua 51 waliuawa na wengine 32 kutoweka na kupelekwa kusikojulikana hadi sasa.

Serikali ya Uingereza ilikuwa imejikita katika kuimarisha Sekta ya Usalama nchini Congo ambapo mpango wa mageuzi ya polisi umepewa kipaumbele na ambapo msaada wa paundi milioni 60 sawa na dola za kimarekani milioni 75 zilitarajiwa kuwasilishwa nchini humo kama sehemu ya mpango wa ufadhili wa miaka mitano ulioanza mwaka 2009.

Kwa mujibu wa ripoti hizo, Operesheni hiyo maarufu kama “Likofi” kwa lugha ya Lingala au Kibao kwa lugha ya Kilswahili, iliyoendeshwa kati ya mwezi Novemba mwaka 2013 na Februari mwaka 2014, iligubikwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu uliotekelezwa na askari polisi wa Congo wakati wa kupambana na vijana maarufu kama Kuluna.

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetupilia mbali ripoti hiyo na kuizungumzia kama ya uongo na yenye lengo la kudhoofisha taasisi zake, jambo amblo awali lilisababishwa kufukuzwa nchini humo kwa mkurugenzi wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya Haki za Binadamu Scott Cambell.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.